Viongozi
wapya wa TUGHE tawi la Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius
Nyerere (JNIA), wakiwa katika picha ya pamoja baada ya uchaguzi.
……………………………………………………………………………………………
ABBAS Rweyumamu amechaguliwa kuwa
mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi wa Afya na Serikali Kuu (TUGHE),
tawi la Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA).
Katika uchaguzi huo uliosimamiwa
na Katibu Mkuu wa TUGHE mkoa wa Dar es Salaam, Gaudence Kadyango ,
ulishirikisha wanachama 36 kutoka idara mbalimbali, ambapo Rweyumamu
alishinda kwa kura 18, akimshinda Teobald Benignus aliyepata kura 17.
Nafasi ya Katibu Mkuu ilikwenda
kwa Thawabu Njeni aliyemshinda Simon Mbogo baada ya kutumika utaratibu
wa kura ya veto, kwa majina yao kuandika kwenye karatasi na Mwakilishi
wa Mkurugenzi wa JNIA, Efatha Lyimo kuokota lililoandikwa jina lake,
baada ya kufungana mara mbili na mpinzani wake kwa kura 18.
Wajumbe wote nane waliogombea na
kupitishwa bila kupingwa ni Tobald Benignus, Simon Mbogo, Rehema Ambali,
Hussein Msuya, Sadik Milulu, Philbery Lyimo, Mwanaheri Omari na
Adventina Rugimbirwa.
Uwakilishi wa vijana umekwenda
kwa Mwanaisha Athuman aliyepata kura 20, na kumshinda Lydia Mwenisongole
aliyepata kura 10; huku nafasi ya uwakilishi wa walemavu umekwenda kwa
Baltazar Kidiga.
Kwa upande wa kamati ya wanawake
Uenyekiti umekwenda kwa Sumayi Ngasani, wakati Mweka hazina kachaguliwa
Stumai Mbato na mjumbe ni Mastidia Ndyomlwango.
Waliochaguliwa kuwa wajumbe wa kamati ya wanawake ni Justa Emmanuel na Joyce Chisongela.
Naye mwakilishi wa DNIA, Lyimo
mbali na kuupongeza uongozi huo, ameutaka kutenda haki na wasiende kuwa
mgombanishi kati ya muajiri na muajiriwa, ila walete ushirikiano baina
ya pande hizo mbili.
Lyimo pia aliwataka viongozi hao
kuweka wazi mapato na matumizi kwa wanachama wake, ili kuepuka migogoro
isiyokuwa ya lazima, na pia waangalie sababu za wanachama wengi
kujiengua kwenye chama hicho.
0 maoni:
Chapisha Maoni