WADAU wa Utalii nchini wameiomba serikali kusitisha
utozwaji wa kodi mpya ya thamani ya ongezeko ,VAT , ambayo ni asilimia
25% kwa kuwa itaua sekta ya utalii nchini.
Hayo yameelezwa leo na wadau wa Utalii kwenye kikao
kilichoitishwa na Chama cha waongoza utalii nchini TATO, kujadili hatua
ya serikali kuwataka kulipa VAT, asilimia 25% kuanzia Julai mosi mwaka
huu.
Wamesema kuwa tayari wageni ambao walitarajiwa kuja nchini
kuanzia Augosti mwaka huu na mwakani wamefuta safari zao kutokana na
kodi hiyo ya VAT asilimia 25% na sasa wanaenda nchi jirani ya Kenya na
hivyo utalii hapa nchini unakufa.
Wamesema wao hawapingi kulipa kodi ila ongezeko hilo ni
kubwa hivyo wanamuomba waziri mwenye dhamana ,Profesa Jmanne Maghembe,
wakaa meza moja kujadili mstakabali huo wa ongezeko la kodi hiyo.
Makamu Mwenyekiti wa TATO., Henry Kimambo, akizungumza
kwenye kikao hicho amesema tayari wameshawasiliana na kamati ya bunge la
jamhuri ya muungano linaloendelea Dodoma, wamekutana na mkuu wa mkoa wa
Arusha Felix Ntibenda, ambako amewaahidi kulishughulikia jambo hilo kwa
kuwasiliana na mawaziri husika.
Amesema wanashangaa kuona serikali ikiongeza VAT na kuua
utalii nchini, wakati Kenya wameondoa kodi hiyo na huu ni wakati wa
ushindani hivyo watalii watakimbilia Kenya .Amesema sekta ya utalii
nchini inachangia pato la taifa kwa asilimia 17% na pia inachangia
fedha za kigeni asilimia 33% .
.Ameongeza kuwa wadau wa utalii hawakatai kulipa kodi bali
ongezeko hilo ni kubwa kiasi kwamba liaathiri sekta nzima ya utalii na
kusababisha makampuni kufunga shughuli hizo.
0 maoni:
Chapisha Maoni