Mbunge Ridhiwani akiwa chumba cha operasheni kuangalia jinsi operesheni ya macho inavyofanywa.picha zote na Omary Mngindo. |
Daktari
akimsikiliza mgonjwa na kumfanyia vipimo huku Mbunge jimbo la Chalinze
Mkoa wa Pwani Ridhiwani Kikwete (mwenye Barghashia) akisubiria zamu yake
kupata vipimo huku akifatilia zoezi linavyoendeshwa.
Daktari akimsikiliza Bibi ayefika kupata matibabu ya macho.
sehemu ya kupata dawa baada ya kufanyiwa vipimo.
MBUNGE
wa Jimbo la Chalinze Halmashauri ya Chalinze Wilaya ya Bagamoyo Mkoa wa
Pwani Ridhiwani Kikwete amewezesha zoezi la upimaji wa macho kwa wakazi
jimboni humo na kupatiwa miwani kwa wakazi zaidi ya 2,000.
Zoezi
hilo ambalo limelenga kuwapatia huduma hiyo wananchi hao ambao
wanakabiliwa na tatizo hilo huku aakikosa uwezo wa kupata huduma
kutokana na hali ya kipato, ambapo Taasisi ya Bilal Muslimu Mission ya
jijini Dar es Salaam imeendesha zoezi hilo katika Kata ya Bwilingu
ambapo mamia ya wananvhi wakijitokeza kupata huduma.
Akizungumza
na waandishi wa habari, Ridhiwani alisema kwamba alikutana na viongozi
wa taasisi hiyo na kufanya nao mazungumzo nao ili wafike kuwapayia
huduma ya kuwapima macjo na kupewa miwani ambapo zoezi hilo limefanyika,
wananchi wamepimwa na kupewa ushauri, mtiba na wemgine kupewa miwani.
"Leo
sio siku ya kuzungumza sana kwani nina furaha kubwa ya kuona wananchi
wamepatiwa huduma ya vipimo, kupatiwa ushauri, kutibiwa macho na wengine
kupatiwa miwani, pia nimewaomba viongozi wa Bilal kuendelea kutoa
huduma ndani ya jimbo lengo wote wafaidike na huduma," alisema
Ridhiwani.
Wananchi wakiwa katika foleni ya kusubiri kupata huduma ya kupima macho.
Kwa
upande wake Mratibu wa Taasisi ya Muslimu Ain Sharifu alisema kuwa
tangu wafike kuanza kuwapatia huduma hiyo wananchi wamejitokeza kwa
wingi kupata huduma, wamewashauri, wamewapatia tiba pia miwani kwa
waliotakiwa kupatiwa na kuwa zaidi ya watu 2,000 wamenufaika na huduma
hiyo.
"Tunashukuru
kwani katika kipinfi chote cha siku tatu za zoezi wananchi wametupatia
ushirikiano mkubwa, taasisi yetu pia inayoa huduma mkoani Morogoro,
tunakuhakikishia Mbunge Ridhiwani kwamba tutaendelea kuwapatia huduma,
tutawaleta mafaktari wetu ili waendelee kuwapatia huduma zaidi," alisema
Sharifu.
Awali
akizungumza katika hafla hiyo ya ufungaji wa utoaji wa huduma hiyo,
diwani wa Kata ya Bwilingu Lucas Lufunga alisema kuwa katika kipindi
chote cha zoezi wananchi wameonesha ushirikiano mkubwa katika mchakato
huo.
0 maoni:
Chapisha Maoni