Mchakato
wa kukamilisha taratibu za kuanza rasmi kwa shughuli za kiutendaji kwa
Ofisi za Mkuu wa wilaya na Manispaa ya Ubungo uko mbio kukamilika.
Kauli
hiyo imetolewa na Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kinondoni ambaye pia ni
Diwani wa Kata ya Ubungo Mhe. Boniface Jacob wakati wa Kikao cha Baraza
la Madiwani leo jijini Dar es Salaam.
Mhe.
Jacob amesema kuwa amearifiwa kuwa taratibu za kugawa rasilimali
zimekamilika kinachosubiriwa tu ni kukamilika kwa suala la upatikanaji
wa majengo ya Ofisi ambayo nayo yako mbioni kupatikana.
Jacob
aliongeza kuwa kukamilika kwa mchakato huo kutaongeza ufanisi katika
uwajibikaji wa kuwatumikia wananchi kwani Manispaa ya Kinondoni imekuwa
ikitoa huduma kwa idadi kubwa sana ya wananchi ila hali watendaji wake
ni wachache hivyo inawagharimu kutekeleza majukumu yao kwa wakati.
Naye
Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Humprey Polepole akitoa salaamu zake baada ya
kukaribishwa katika Baraza hilo alisema kuwa wakati wowote shughuli za
kiutendaji katika Wilaya ya Ubungo zitakuwa zikitolewa katika Ofisi zake
kwani mchakato umekwisha kamilika.
“Nifuraha
yangu kuwa leo nipo hapa na watumishi wenzangu wengine inawezekana
tukawa Ofisi moja katika wilaya yangu ya Ubungo, kwani nimearifiwa kuwa
kila kitu kimekamilika hadi mgawanyo wa watumishi,” alisema Polepole.
Aliongeza
kuwa anayo imani kuwa kazi iliyombele yake ni kuwatumikia wananchi wa
Ubungo kwa kuwaletea maendeleo hivyo ni vyema akapata ushirikianao kwa
wadau wote bila kujali itikadi zao.
Kuna namna mbili zipo zinazitwa “Political Power “ na zile “Political Development”; nisema tu
Kuna namna mbili zipo zinazitwa “Political Power “ na zile “Political Development”; nisema tu
0 maoni:
Chapisha Maoni