Mkuu
wa wilaya ya Kilolo Bi Asia Abdalah katikati akiwa na watendaji
wa kituo cha afya Kilolo kushoto ni mganga mkuu wa kituo hicho Dr
Seleman Hassan na kulia ni Ephlon Msuva.
MKUU
mpya wa
wilaya ya Kilolo mkoani Iringa Bi
Asia Abdalah ameanza kazi ya kumwakilisha Rais Dr John Magufuli kwa
kupima Virusi vya UKIMWI
kama njia ya kuhamasisha
wananchi wa wilaya ya
Kilolo kupima afya zao
.
Akizungumza baada ya kupima na kutembelea kukagua huduma zinazotolewa
kituo cha afya cha
Kilolo leo asubuhi ,mkuu huyo
wa wilaya alisema
kuwa ni siku yake ya
pili ya kuanza kazi ndani ya
wilaya hiyo ya Kilolo ila mbali ya siku ya
kwanza kufuatilia utekelezaji wa
agizo la Rais Dr Magufuli la madawati
siku yake ya pili ameamua kutembelea
kituo cha afya
kuona huduma zinazotolewa pia kupima HIV kama njia ya
kuhamasisha jamii.
Mkuu huyo
alisema kuwa mkoa wa Iringa
kwa takwimu zilizopo
unaonyesha kuwa ni miongoni
mwa mikoa ambayo
ipo juu katika maambukizi ya virusi
vya UKIMWI na wilaya
yake ya Kilolo ni
miongoni mwa wilaya
zenye maambukizi ya VVU hivyo pamoja na kutembelea na
kupata maelezo ya mikakati
ya wilaya katika
kupambana na maambukizi mapya ya VVU amelazimika kupima VVU kama sehemu ya
kuhamasisha jamii ya Kilolo na
pia kuonyesha mfano kwa jamii.
“
Nawaomba wananchi wa
Kilolo kujenga utamaduni
wa kujua afya
zao kwa kupima VVU pamoja na magonjwa mengine ambukizi ili
kuwa na wananchi wenye afya
bora “
Alisema kuwa
serikali imeweka utaratibu mzuri
wa kuwapatia dawa
wale wote watakaobainika kuwa na maambukizi ya VVU na
kuwa lengo ni kuona
hakuna mtanzania ambaye anapoteza
maisha kwa kukosa
dawa hizo za kupunguza makali
ya virusi vya
UKIMWI .
Aidha aliwataka
wauguzi na madaktari
katika wilaya hiyo
kuendelea kufanya uhamasishaji na elimu kwa jamii ili
wazidi kujitokeza kuchunguza
afya zao .
Pia
alisema amefurahishwa na mkakati wa wilaya ya Kilolo wa kujenga
Hospitali yake ya wilaya katika makao makuu ya wilaya hiyo na
kuwa tayari wilaya imetenga ardhi kwa ajili ya ujenzi huo .
Alisema
suala la kusogeza huduma za afya karibu na wananchi ni moja kati
ya sera chama cha mapinduzi (CCM) na kwa upande wake atahakikisha
ujenzi huo unakamilika .
Kwa upande
wake Mganga wa kituo hicho
cha afya Kilolo Dr Seleman Hassan
alisema wilaya hiyo
imekuwa na mikakati mbali mbali ya
kupambana na maambukizi ya VVU
na kuwa wakati wa mbio za
mwenge wilayani hapo jumla ya
watu 200 walijitokeza kupima VVU na kati yao watu 19
waligundulika kuwa na maambukizi ya
VVU na tayari
wameingizwa katika huduma ya kupewa
dawa za ARVS
|
0 maoni:
Chapisha Maoni