Jumamosi, 16 Julai 2016

HALMASHAURI YA MANISPAA YA IRINGA YAIBUKA KIDEDEA TUZO YA USAFI WA MAZINGIRA NCHINI

Postedy by Esta Malibiche on July 16.7.2016 News


Mstahiki Meya wa Manispaa ya Iringa Alex Kimbe akizungumza na wandishi wa Habaria hawapo pichani








HALMASHAURI ya Manispaa ya Iringa imewataka wananchi wake kuendelea kutanza mazingira kwa kupanda miti na kudumisha usafi katika maeneo yanayowazunguka na kufukia madindwi ya mazalia ya mbu ili Iringa iendelee kuwa katika hali ya usafi.

Akizungumza  leo  na BLOG YA KALI YA HABARI  Mstahiki Meya wa Manispaa ya Iringa kwa tiketi ya chama cha democrasia na maendeleo chadema ambae ni Diwani wa kata ya Isakalilo, Alex Kimbe alisema alisema  kuwa  kushinda  kwa  tuzo  hiyo  ya usafi kwa  Halmashauri  ya  Manispaa ya  Iringa ni heshima  kubwa  na  kuwa pamoja na kujipongeza kwa  kuongoza  kwa  usafi  kwa Halmashauri  za Manispaa nchini  bado   kazi  kubwa ni  kuona  mji wa Iringa  unaendelea   kuongoza  katika  usafi .

Akielezea  kuhusu  aina ya  tuzo  zinazotolewa kwa  washindi  alisema  kuwa  kuna  haja  ya   wizara   husika  kuboresha aina  ya  zawadi   hizo ili  ziwe  zenye  tija  zaidi kuliko  kuendelea  kutoa  pikipiki ambazo  si msaada katika  kusaidia  usafi . Ni bora  wizara  ingekuwa inatoa  zawadi  ya gari la taka kwa  washindi ama  kutoa  vyombo   vya  kuhifadhia  takataka  ambavyo  ni changamoto  kubwa kwa  Halmashauri  kuvipata .
 '''Ili kuongeza  kasi ya  usafi katika Halmashauri zetu,Wizara ya  Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto ambao  ni  waratibu  wa mashindano hayo  kuangalia  zawadi   wanazozitoa  ziwe  msaada  wa   kusaidia  kuboresha  usafi  wa Mazingira  katika Halmashauri   hiyo .Zawadi  za ushindani  zingekuwa ni vifaa vya kusombea taka ,sababu pikipiki  haisaidii  kusomba  uchafu katika madampo ambayo  yanatumika   kutupa  taka’’’’’’alisema kimbe
 Pia  alisema  moja kati ya mkakati ambao  umewekwa na Manispaa ya  Iringa ni  kuendelea  kuitumia  jumamosi ya  mwisho  wa  mwezi   kwa  ajili ya wananchi   wote  kutoka kufanya  usafi katika maeneo yao na  kuwa  mwananchi  atakayepuuza agizo hilo atatozwa  faini ya Tsh  50,000.Mkakati  mwingine ni  kuweka  vyombo  vingi  zaidi vya  wananchi  kutupa uchafu  vyombo  vitakavyofungwa  kando kando ya  barabara  na  baada ya  hapo  vikundi  vya vijana  vitapewa  kazi ya  kukamata   wote  wanaotupa uchafu  ovyo  na  kuwachukulia hatua  kali ikiwa ni  pamoja na  kutozwa faini.
 Kwa upande wake diwani wa kata ya Nduli kwa tiketi ya chama cha Mapinduzi ccm Bashir Mtove aliipongeza  jitihada  mbali mbali  zinazoendelea  kufanywa na  wananchi wa Manispaa ya  Iringa kwa  kuendelea  kuuweka  mji  huo katika  hali ya  usafi  zaidi.


 Mtove alisema kuwa Halmashauri  ya Manispaa ya  Iringa  imeshika  nafasi ya  kwanza  kitaifa  ya  usafi  wa mazingira  kutokana na wananchi wake kuwa wasikivu na watii,na kusema kuwa ushindi huu umeleta heshima kubwa ndani ya mkoa na Taifa kwa ujumla
 Ushindi huu si wa wanamanispaa pekee bali ni wa mkoa na Taifa kwa ujumla,hivyo ninawaomba wanaIringa tuendelee kudumisha usafgi katika mazingira yanayotuzunguka ili tuendelee kushika nafasi kubwa zaidi’’’’’’alisema Mtove

0 maoni:

Chapisha Maoni