Shirikisho
la Mpira wa Miguu Rwanda (FERWAFA), limeahirisha mchezo wa kirafiki wa
kimataifa kati ya timu ya taifa ya wanawake ya Rwanda dhidi ya wageni,
Tanzania ‘Twiga Stars’ uliokuwa ufanyike Jumapili Julai 17, 2016.
Mchezo
huo uliandaliwa na FERWAFA na Rais Paul Kagame alipendekeza mchezo huo
kuwa sehemu ya burudani kwa wakuu mbalimbali wa nchi za Afrika
wanaotarajiwa kuwa na mkutano wa viongozi hao kuanzia kesho Julai 14,
2016.
Kwa
mujibu wa barua ya Rais wa FERWAFA, Nzamwita Vincent ya Julai 12, 2016
kwenda Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), sababu za kuahirisha
mchezo huo ni ratiba ya mkutano huo wa 27 wa wakuu nchi.
“Tunasikitika
kuwataarifu kuwa ile ratiba ya kuwa na mchezo wa kirafiki kati ya
Rwanda na Tanzania, imefutwa. Tunaomba radhi kwa taarifa hii ya ghafla
ambayo iko nje ya uwezo wetu inayowafikia huku tukijua kwamba mlikuwa
tayari mmeandaa timu kwa ajili ya mchezo,” ilisema sehemu ya barua hiyo.
“Hata hivyo tunaahidi kuendelea kufanya mawasiliano ili kupanga tarehe nyingine ya kufanyika mchezo huo,” ilisisitiza barua.
Taarifa
hiyo imekuja wakati tayari Twiga Stars ilikuwa imeanza maandalizi ya
kutosha kwa mchezo huo ambao ulianza kuvutia mamia ya mashabiki wa mpira
wa miguu wan chi za Afrika Mashariki.
Shirikisho
la Mpira wa Miguu Rwanda (FERWAFA), limeahirisha mchezo wa kirafiki wa
kimataifa kati ya timu za wanawake za Tanzania ‘Twiga Stars’ na wenyeji
Rwanda uliokuwa ufanyike Jumapili Julai 17, 2016.
Mchezo
huo uliandaliwa na FERWAFA na Rais Paul Kagame alipendekeza mchezo huo
kuwa sehemu ya burudani kwa wakuu mbalimbali wa nchi za Afrika
wanaotarajiwa kuwa na mkutano wa viongozi hao kuanzia kesho Julai 14,
2016.
Kwa
mujibu wa barua ya Rais wa FERWAFA, Nzamwita Vincent ya Julai 12, 2016
kwenda kwa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), sababu za
kuahirisha mchezo huo ni kuingiliana kwa ratiba ya mkutano huo wa 27 wa
wakuu nchi za Afrika.
“Tunasikitika
kuwataarifu kuwa ile ratiba ya kuwa na mchezo wa kirafiki kati ya
Rwanda na Tanzania, imefutwa. Tunaomba radhi kwa taarifa hii ya ghafla
ambayo iko nje ya uwezo wetu inayowafikia huku tukijua kwamba mlikuwa
tayari mmeandaa timu kwa ajili ya mchezo,” ilisema sehemu ya barua hiyo.
“Hata
hivyo tunaahidi kuendelea kufanya mawasiliano ili kupanga tarehe
nyingine ya kufanyika mchezo huo,” ilisisitiza barua iliyosainiwa na
Nzamwita Vincent.
Taarifa
hiyo imekuja wakati tayari Twiga Stars ilikuwa imeanza maandalizi ya
kutosha kwa mchezo huo ulioanza kuvutia mamia ya mashabiki wa mpira wa
miguu wa ncza Afrika Mashariki na kati.
0 maoni:
Chapisha Maoni