Mbunge
wa Nzega Vijijini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dk. Hamisi Kigwangalla akielekea
katika jengo lililoezuliwa na upepo la shule ya Iyombo Itima iliyo Kata
ya Budushi, Jimbo hilo la Nzega Vijijini.
Jengo hilo linavyookena baada ya kuezuliwa na upepo
Baadhi ya wanafunzi wa shule ya Msingi Iyombo Itima wakiwa wanasomea nje baada ya darasa lao kuezuliwa na upepo
Nje ya jengo hiloMbunge
wa Nzega Vijijini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dk. Hamisi Kigwangalla akiangalia
darasa ambalo nalo hali yake si nzuri baada ya sakafu yake kuchakaa
Mbunge
wa Nzega Vijijini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dk. Hamisi Kigwangalla akizungumza
na wananchi wa Kijiji cha Iyombo Itima (Hawapo pichani) wakati
alipowatembelea kutoa shukrani zake baada ya kumchagua kwenye uchaguzi
uliopita. Kulia ni Diwani wa Kata ya Budushi, Mh. Omary Maganga (Picha
zote na Andrew Chale,
Mbunge
wa Nzega Vijijini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dk. Hamisi Kigwangalla amepokea ombi
la kusaidia ukarabati wa jengo la shule ya Msingi Iyombo Itima iliyopo
Kata ya Budushi ambayo iliezuliwa na upepo mkali katika kipindi cha mvua
za masika hali iliyopelekea wanafunzi kusomea nje.
Dk.
Kigwangalla ambaye yupo ziarani katika jimbo lake hilo kwa ajili ya
kuwashukuru wananchi kwa kuweza kumchagua ili awawakilishe Bungeni,
ambapo katika ziara yake hiyo ya kushukuru katika Kata hiyo, Diwani
Omary Maganga alimuomba Dk. Kigwangalla kuweza kusaidia ukarabati wa
jengo hilo ili kuwaondolea adha ya wanafunzi kusomea juani.
Hata
hivyo, Dk. Kigwangalla alipokea ombi hilo na kuahidi kutoa kiasi cha
Sh. Milioni tatu kwa ajili ukarabati huo ambao utaenda sambamba na
ukarabati wa sakafu katika moja ya madarasa ya shule hiyo baada ya
kushuhudia hali hiyo baada ya kutembelea.
Dk.
Kigwangalla yupo jimboni kwa ziara hiyo ya kuwashukuru wananchi ambapo
anatembelea Kata mbalimbali za Jimbo na kutoa shukrani hizo ikiwemo
kutoa misaada na michango aliyowaahidi.
0 maoni:
Chapisha Maoni