MKUU wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji
Jumanne Mtaturu mapema leo amehutubia waumini wa dini ya kiislamu katika
msikiti wa Ijumaa kuu Wilayani humo .
Kwa kutambua umuhimu wa Elimu nchini,
Mtaturu alichangia kiasi cha Tsh.Mill.1
kwa ajili ya ujenzi wa shule ya asekondari itakayokuwa chini ya msikiti
huo.
Katika hotuba yake aliwataka wananchi
kuchangia shughuli za maendeleo ili wilaya hiyo iweze kusomba mbele
kimaendeleo.
Ninawaomba wananchi tushirikiane pamoja ili tuweze kutatua changamoto mbalimbali zinazoikabili Wilaya yetu.
Nao Wananchi walimuunga mkono mkuu
huyo wa wilaya kwa kuchagia kiasi cha Tsh. 255,000 na kufanya kufikisha milioni
1, 255,000 kwa ajili ya kuanza ujenzi wa shule hiyo.








0 maoni:
Chapisha Maoni