Ijumaa, 6 Mei 2016

ZANZIBAR YAADHIMISHA SIKU YA WAKUNGA DUNIANI

Z1Waziri wa Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi Hamad Rashid Mohammed ambae alikuwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya siku ya Wakunga Duniani akibadilishana mawazo na Mwenyekiti wa Baraza la Wauguzi na Wakunga Zanzibar Profesa Amina Abdulkadr, (kulia) Waziri wa Afya Mahmoud Thabit Kombo na (kushoto) Naibu Katibu Mkuu  Wizara hiyo Halima Maulid Salum.
Z2Mwenyekiti wa Baraza la Wauguzi na Wakunga Zanzibar Profesa Amina Abdulkadr akisoma risala ya wakunga katika maadhimisho ya siku ya Wakunga Duniani yaliyofanyika Ukumbi wa Sanaa Rahaleo Mjini Zanzibar.
Z3Mwakilishi wa Shirika linaloshughulikia Idadi ya watu (UNFPA) akitoa salamu za Shirika hilo kwenye maadhimisho ya siku ya Wakunga Duniani yaliyofanyika Ukumbi wa Sanaa Rahaleo Mjini Zanzibar.
Z4Waziri wa Afya Mahmoud Thabit Kombo akimkaribisha Mgeni rasmi Waziri wa Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi Hamad Rashid Mohammed katika maadhimisho ya siku ya Wakunga Duniani.

0 maoni:

Chapisha Maoni