Ijumaa, 6 Mei 2016

BONDIA VICENT MBILINYI AJITAHALISHA NA MPAMBANO WAKE WA JUNE 4

………………………………………………………………
Na Mwandishi Wetu
BONDIA Vicent Mbilinyi ameingia kambini rasmi kwa ajili ya mazoezi yake ya mpambano ujao atakapo zipiga na
Bondia Msafiri Haule katika mpambano wa raundi sita utakaofanyika juni 4 mwaka uhu katika ukumbi wa uwanja wa ndani wa taifa
Mbilinyi aliye chini ya kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila ‘Super D’ amejizatiti kushinda mpambano wake uho kwa kuwa amefanya mazoezi kwa mda mrefu na ajapigana katika jiji la Dar es salaam kwa mda hivyo mashabiki wake wakae mkaa wa kufuraia siku hiyo
aliongeza kwa kusema kuwa Mashabiki wake wategemee ushindi wa K.O mbaya sana aliongeza kwa kusema kuwa kama mashabiki watakumbuka mpambano wangu wa mwisho nilivyo msambalatisha Deo Njiku kwa K,O hivyo mwendeezo wangu utakuwa hivyo hivyo kwa huyo bondia
nae kocha wa kimataifa Rajabu Mhamila ‘Super D’ anaemnowa Mbilinyi amesema kuwa bondia huyo yupo fiti ata kama mpambano utapigwa leo kwa kuwa amefanya mazoezi ya muda mrefu na yakutosha akiwa chini ya kocha huyo ambaye jukumu lake alishii tu kwa ukocha pamoja na kumtangaza nje na ndani ya nchi na kumtafutia mapambano mbali mbali ambayo yanamwezesha kuendeleza kipaji chake hicho
mbali na mpambano uho siku hiyo kutakuwa na mapambano ya mabondia wa uzito wa juu nchini siku hiyo itajulikana kama  ‘Usiku wa Mahavy Weight’ ambapo bondia Ashiraf Selemani kutoka Zanzibar atapanda uringoni kuzichapa na Mthailand wakati bondia mwingine Amour Mzungu kutoka Zanziba atazipiga na Japhert Kaseba
na mapambano mengine mbalimbali yatakayosindikiza usiku huo wa mabondia wa uzito wa juu nchini

0 maoni:

Chapisha Maoni