Mwamuzi Joseph Odartei Lamptey,
Jumamosi Mei 7, 2016 anatarajiwa kuwa mwamzi wa kati katika mchezo wa
kimataifa kuwania Kombe la Shirikisho Barani Afrika utakaozikutanisha
timu za Young Africans ya Dar es Salaam, Tanzania na GD Sagrada
Esperanca ya Angola.
Lamptey kutoka jiji la Accra,
Ghana atasaidiwa na raia wenzake wa nchi hiyo kuchezesha mchezo huo Na.
99. Mwamuzi Msaidizi Na. 1 (line 1) ni David Laryea wakati Mwamuzi
Msaidizi Na. 2 (line 2) ni Malik Alidu Salifu.
Mwamuzi Msaidizi mezani (Fourth
Official) ni Cecil Amately Fleischer huku Kamishna wa mchezo huo, akiwa
ni Asfaw Luleseged Begashaw wa Ethiopia.
Viingilio na upatikanaji wa
tiketi utatangazwa kesho Ijumaa Mei 6, 2016 na uongozi wa klabu ya Young
African mara baada ya mkutano kati ya makocha wa timu zote mbili.
Mkutano wa makocha hao utafanyika saa 5.00 mchana kwenye Ukumbi wa
mikutano wa TFF.
Mwamuzi Joseph Odartei Lamptey,
Jumamosi Mei 7, 2016 anatarajiwa kuwa mwamzi wa kati katika mchezo wa
kimataifa kuwania Kombe la Shirikisho Barani Afrika utakaozikutanisha
timu za Young Africans ya Dar es Salaam, Tanzania na GD Sagrada
Esperanca ya Angola.
Lamptey kutoka jiji la Accra,
Ghana atasaidiwa na raia wenzake wa nchi hiyo kuchezesha mchezo huo Na.
99. Mwamuzi Msaidizi Na. 1 (line 1) ni David Laryea wakati Mwamuzi
Msaidizi Na. 2 (line 2) ni Malik Alidu Salifu.
0 maoni:
Chapisha Maoni