Jumatatu, 16 Mei 2016

SERIKALI KUPITIA WIZARA YA KILIMO,MIFUGO NA UVUVI YAPIGA MARUFUKU VIPIMO VYA LUMBESA


Waziri Mwigulu  akiwahutubia  wananchi  wa Miuna kata ya Mbekese jimboni kwake Iramba
waziri Nchema akitoa msisitizo kwa   wakulima  kuacha  kuuza mazao kwa  vipimo batili 
Baada ya mkutano wa hadhara waziri Mwigulu alipata nafasi ya kusalimiana na wazee wa kijijini kwake Makunda Iramba baada ya mkutano wake wa saba

Waziri wa kilimo,Chakula na uvuvi Bw Mwigulu Nchemba aagiza hatua kuchukuliwa kwa wanunuzi wa mazao wanaonunua mazao ya wakulima kwa vipimo batili (Lumbesa)vinavyowanyonya wakulima.

Kuwa kuanzia sasa ni marufuku wafanyabiashara kuchumbia mazao shambani kama ambavyo wamekuwa wakiwahadaha wakulima kwa kununua viazi katika matuta na mazao mengine yakiwa machanga shambani.

Waziri Nchemba  ambae ni mbunge wa jimbo la Iramba mkoani Singida alitoa agizo hilo leo wakati wa mikutano yake  ya hadhara kwa ajili ya kuwashukuru wananchi wake kwa kumchagua bila kufanya kampeni .

Alisema lengo la serikali kuona wakulima wananufaika na kilimo hivyo lazima wanunuzi w mazao kununua mazao kwa vipimo sahihi na kuacha kununua mazao kwa vipimo batili maarufu kama Lumbesa ambavyo serikali ilikwisha piga marufuku vipimo hivyo.

Waziri huyo aliagiza viongozi wa serikali ya vijiji kata na wilaya kuwasaidia wakulima kuuza mazao yao kwa vipimo sahihi na kuwachukulia hatua wafanyabiashara wanaowaibia wakulima

" wapo baadhi ya wafanyabiashara
 wanawarubuni wakulima kununua mazao yakiwa shambani pasipo kuvunwa na tabia hii si ipo hapa Iramba pekee bali ipo karibu nchi nzima kule Mbeya watu wananunua ndizi na viazi vikiwa shambali pia kwa mikoa mingine ni hivyo hivyo"

Waziri Nchemba alisema tabia hiyo ya kunyonya wakulima katika serikali hii ya awamu ya tano haitavumilika wahusika wote wanaotesa wakulima.

Pia alitaka viongozi wa serikali ngazi za vijiji kote nchini kuwachukulia hatua wanunuzi wa mazao ya wakulima kama mahindi na mengime yanayopimwa katika ndoo ambao wanatembea na ndoo zao ambazo ni maalum kwa kuwapunja wakulima.

" Wapo baadhi ya wafanyabiashara wanatembea na ndoo zao ambazo wamevimbisha kwa mchanga wa moto ama maji ya moto maalum kwa kuwapunja wakulima ......sasa naagiza viongozi wa serikali za vijiji kote nchini wananchi watumie ndoo zao kuuza mazao"

Alisema ni vema wafanyabiashara ambao ni wananchi wa vijiji husika kuwasaidia wakulima wa hapa nchini kwa kununua mazao kwa vipimo sahihi na kama ni kuwapunja kwa ajili ya kutafuta faida waende kuwaibia wafanyabiashara wa nje na maeneo ya wakulima.

" kwa ngunia la mahindi ama maharage ni debe sita na sio debe saba ama nane ambazo wamekuwa wakiwaibia na alizeti ngunia ni debe saba si zaidi ya hapo"































0 maoni:

Chapisha Maoni