Mkuu wa wilaya
ya Iringa Richard Kasesela amewataka viongozi wa dini ya kiislamu nchini kuishi
kwa kufuata maadili ya kiislamu kama Qur’an tukufu inavyosema ili waweze kuwaongoza waumini wao .
Akizungumza na viongozi wa Balaza la waislamu Iringa
Mjini katika wakati akifungua mkutano wa Bakwata uliofanyika jana mkoani hapa na kuhudhuriwa na wajumbe wa mbalimbali,Kasesela
alisema kiongozi anatakiwa awe mcha
mungu,muadilifu,mkweli,mwenye huruma kwa waumini wake,mkweli na asiyethubutu
kujilimbikizia mali kwa kutumia wajibu au cheo cha uongozi alichonancho kwa
manufaa yake binafsi.
Kasesela aliitoa kauli hiyo
kufuatiwa kujiondoa kwa baadhi ya viongozi wawili ya bakwata Iringa mjini
na kushinikiza kufanyika uchaguzi upya,
ambao ulitakiwa ufanyike jana jumapili kwa madai yao binafsi kuwa uongozi wa
bakawata uliopo si halali,ndipo jeshi la polisi lilitupilia mbali omb hilo na
kusitisha kuwepo kwa uchaguzi huo ambao ni batili hadi taarifa itakapotoka
bakwata Taifa
Alisema kiongozi anatakiwa
daima kuwa mtumishi wa wale waliomuweka
katika uongozi,kwa kuwa mnyenyekevu,mwenye kuwahurumia wale anaowaongoza na
mwenye kuwapendelea analolipendelea katika nafsi yake
Alisema kipimo cha kiongozi
mzuri ni uadilifu,kiongozi mzuri akiwa muadilifu huwa khalifa wa Alla[s.s] na
akiwa si muadilifu huwa khalifa wa shetani,hivyo kwa kuwa uadilifu unasisitizwa
katika Qur’an inapaswa jamii na waislamu kwa ujumla kuzingatia agizo hilo kwa
vitendo.
0 maoni:
Chapisha Maoni