Jumatatu, 16 Mei 2016

Waajiri hakikisheni wafanyakazi wapo kwenye vyama


Naibu Waziri wa Kazi, Vijana na Ajira, Antony Mavunde amesema suala la wafanyakazi kuwa na vyama vya wafakazi kwenye taasisi wanazofanya kazi ni jambo la kikatiba na nilazima waajiri wazingatie hilo.
Mavunde ameyasema hayo Bungeni Dodoma alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Vwawa Mkoani Mbeya , Japhet Hasunga wa (CCM) aliyetaka kujua msimamo wa Serikali juu ya waajiri ambao hawataki wafanyakazi wao kujiunga vyama vya wafanyakazi.
Naibu Waziri Mavunde amesema kwamba kwa mujibu wa sheria ya kazi namba 6 ya mwaka 2004 ni haki ya wafanyakazi kuwa kwenye vyama na mwajiri yoyote ambaye anakataa jambo hilo anakiuka katiba na atachukuliwa sheria stahiki.
Aidha Naibu Waziri amewataka wafanyakazi ambao hawapo katika vyama vya wafanyakazi kutambua ni jambo ambalo ni haki yao na linatambulika kwa mujibu wa sheria za nchi.

0 maoni:

Chapisha Maoni