Jumatano, 11 Mei 2016

RAIS DK. MAGUFULI AFANYA UTEUZI WA WENYEVITI WA BODI ZA TAFORI NA TTB

logoUTEUZI WA WENYEVITI NA WAJUMBE WA BODI YA WAKURUGENZI WA SHIRIKA LA MAKUMBUSHO YA TAIFA, TAASISI YA UTAFITI WA MISITU TANZANIA (TAFORI) NA BODI YA UTALII TANZANIA (TTB).
……………………………………………………………………………………
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amefanya uteuzi wa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Makumbusho ya Taifa, Bodi ya Taasisi ya Utafiti wa Misitu Tanzania (TAFORI) na Bodi ya Utalii Tanzania (TTB).
Katika uteuzi huo Mhe. Rais amemteua Bi. Anna Abdallah (Mbunge Mstaafu) kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Makumbusho ya Taifa, Dkt. Felician Kilahama (Mbobezi katika fani ya Misitu) kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi ya Utafiti wa Misitu Tanzania (TAFORI) na Jaji Mstaafu Thomas Mihayo kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB).
Kufuatia uteuzi huo wa Mhe. Rais, Waziri wa Maliasili na Utalii kwa mamlaka aliyonayo chini ya Sheria ya Shirika la Makumbusho ya Taifa Sura ya 281 kifungu cha 4(2) kikisomwa pamoja na Jedwali aya ya (1a) amewateua wafuatao kuwa Wajumbe wa Bodi hiyo;
  1. Amina Amer Issa, Mkurugenzi wa Makumbusho, Nyaraka na Mambo ya Kale Zanzibar.
  2. Ali S. Mcharazo, Mkurugenzi wa Tanzania Library Services, Dar es Salaam.
  3. Godius Kahyala, Dean, College of Arts and Social Sciences University o,f Dar es Salaam.                                                           
  4. Thomas J. Lyimo, Dean, Faculty of Science University of Dar es Salaam.
  5. Oswald Masebo, Mhadhiri, Mkuu wa Idara ya Historia, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
  6. Lota Melamari, Consult, Management of Natural Resources and       Environment and Coordinator of Tanga Botanical Gardens, Arusha.
  7. Anna M. Kishe, Mtaalam wa lugha za Kiswahili na Kiingereza na       Mhadhiri katika Chuo Kikuu Huria cha Tanzania, Dar es Salaam.
  8. Donatius M. Kamamba, Mkurugenzi wa Mambo ya Kale, Wizara ya Maliasili na Utalii.
Aidha, kwa mamlaka aliyonayo chini ya Sheria ya Taasisi ya Utafiti wa Misitu Tanzania (TAFORI) Sura ya 277 kifungu cha 6(2) kikisomwa pamoja na Jedwali la 2 (1)(a), Mhe. Waziri amewateua wafuatao kuwa Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa taasisi hiyo;
  1. Salim Maliondo, Profesa wa Biologia ya Misitu Chuo  Kikuu cha Kilimo Sokoine, Morogoro.
  2. Susana Augustino, Mhadhiri Mwandamizi matumizi ya mazao ya misitu, Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine, Morogoro.
  3. Deusdedit Bwoyo, Kaimu Mkuruenzi Msaidizi, Maendeleo ya Misitu, Wizara ya Maliasili na Utalii, Dar es Salaam.
  4. Dismas L. Mwaseba, Mhadhiri Mwandamizi, Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine, Morogoro.
  5. Charles Maguta Kajege, Business Consulatant (Finance), Dar es Salaam.
  6. Lemayon Melyoki Mkurugenzi, Shule ya Ujasiriamali, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
  7. Tuli S. Msuya, Katibu Tawala, Mfuko wa Misitu Tanzania, Wizara ya Maliasili na Utalii, Dar es Salaam.
  8. Emma Liwenga, Mtafiti Mwandamizi, Taasisi ya Tathmini ya Maliasili (IRA), Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
  9. Lawrence Mbwambo, Kaimu Mkurugenzi Mkuu, Taasisi ya Utafiti wa Misitu Tanzania (TAFORI), Morogoro.
Pia, kwa mamlaka aliyonayo chini ya Sheria ya Bodi ya Utalii Tanzania Sura ya 364 kifungu cha 3(2) kikisomwa pamoja na Jedwali 1(2), Mhe. Waziri amewateua wafuatao kuwa Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa taasisi hiyo;”
  1. Ibrahim Mussa, Mkurugenzi wa Masoko, TANAPA
  2. Balozi Joseph Sokoine Mkurugenzi Idara ya Ulaya na Amerika, Wizara ya Mambo ya Nje, Afrika Mashariki Kikanda na Kimataifa.
  3. Mark Leveri, Mtaalam wa kutengeneza filamu na matangazo ya video, Ex. Tanzania Film Company.
  4. Richard Rugimbana, Mtendaji Mkuu Tanzania Confederation of Tourism (TCT).
  5. Zabein Muhaji Mhita, Mbunge Mstaafu na Mkurugenzi wa Elimu ya  Msingi Mstaafu.
  6. Agustine Kungu H. Olal, Kamishna Msaidizi wa Sera na Uchumi, Wizara ya Fedha na Mipango.
Uteuzi wa Wenyeviti na Wajumbe hao ni wa muda wa miaka mitatu kuanzia tarehe 24/04/2016 hadi tarehe 23/04/2019.
            IMETOLEWA NA:
Angelina E.A. Madete
KAIMU KATIBU MKUU
WIZARA YA MALIASILI NA UTALII
10 Mei, 2016

0 maoni:

Chapisha Maoni