Jumatano, 11 Mei 2016

PIZZA HUT YAFUNGUA MGAHAWA NCHINI TANZANIA KWA KUPELEKA PIZZA KWENYE KILELE CHA MLIMA KILIMANJARO


1Balozi wa Markani nchini Balozi Mark Childress katikati akishirikiana pamoja na Bw. Vikram Desai Mkurugenzi wa Dough Works Ltd, Vikram Desai na Mkurugenzi wa Pizza Hut  Afrika, Randall Blackford Afrika, Randall Blackford kulia kukata utepe  kuzindua rasmi mhagawa huo uliopo jengo la Mkuki Barabara ya Nyerere jijini Dar es salaam leo.
2Balozi wa Markani nchini Balozi Mark Childress akipata maelezo kutoka kwa  Bw. Vikram Desai Mkurugenzi wa Dough Works Ltd, Vikram Desai mara baada ya kuzindua rasmi mgahawa wa Pizza Hut uliopo jengo la Mkuki jijini Dar es salaam.
3Balozi wa Markani nchini Balozi Mark Childress akizungumza na wageni waalikwa katika uzinduzi huo uliofanyika leo.
4
Baadhi ya wageni mbalimbali walioalikwa katika uzinduzi huo wa mgahawa wa Pizza Hut.
5Bw. Vikram Desai Mkurugenzi wa Dough Works Ltd, Vikram Desai akizungumza na wageni waalikwa na kumkaribisha Balozi wa Marekani Mark Childress ili kuzungumza na wageni waalikwa.
………………………………………………………………………………………………………………………..
Huduma ya kupeleka pizza kileleni itatimiza rekodi ya dunia ya Guinness, kwa kutoa pizza kwenye urefu wa juu kabisa katika ardhi, ili kuashiria ufunguzi wake nchini Tanzania.
*****                  ******                     *******
 Kwa kutambua kuingia katika nchi yake ya mia moja, Pizza Hut, ambayo ni sehemu ya Yum! Brands, Inc (NYSE: YUM) na ambayo ni kampuni kubwa duniani ya mgahawa wa pizza, imesherekea ufungunzi wa mghahawa kwa kupeleka pizza katika kilele cha mlima Kilimanjaro nchini Tanzania. Kwa kupeleka pizza hii inaweka rekodi ya dunia ya Guinness, kwa kutoa huduma ya kupeleka pizza katika urefu mkubwa, juu ya ardhi wenye urefu wa zaidi ya futi 19,000.
Meneja Mkuu wa kampuni ya Pizza Hut kwa Afrika, Randall Blackford, timu ya wafanyakazi wa Pizza Hut na baadhi ya wataalamu waangalizi, walipanda hadi kileleni mwa mlima Kilimanjaro kwa siku tano ili kuweka rekodi ya dunia. Blackford na timu kwa pamoja walishiriki kula pizza kubwa inayojulikana kama pepperoni juu ya kilele cha mlima katika kusherehekea mwendelezo wa kupanuka kwa Kampuni kimataifa. Mshauri kutoka rekodi ya dunia ya Guinness alikuwepo nchini Tanzania ili kuthibitisha kwamba Pizza Hut kweli imeweka rekodi kwa kutoa huduma ya kupeleka pizza kwenye urefu wa juu kabisa katika ardhi.
Si tu kwamba timu imeweka rekodi za dunia za Guinness, pia wamechangia kiasi cha shilingi za kitanzania milioni 15 (karibu dola za kimarekani 7,000) kwa Shule ya Msingi Msasani jijini Dar Es Salaam,Tanzania kama njia ya kuonyesha dhamira yao ya kusaidia jamii ambazo zimewazunguka. Fedha hizo zitasaidia kufanya matengenezo mbalimbali ya shule kwa wanafunzi 1,300 na kutoa mafunzo kwa walimu wao.
“Tunayofuraha kubwa kuileta Pizza Hut nchini Tanzania na tunaamini hakuna njia bora ya kusherehekea nchi yetu ya 100 zaidi ya kuweka rekodi ya dunia kwa kutoa huduma ya kupeleka pizza juu kabisa ya ardhi kwenye mlima Kilimanjaro, “alisema Milind Pant, Rais wa Pizza Hut kimataifa. “Pizza Hut iko njiani kuwa ni mgahawa unaopendwa zaidi na kukua kwa kasi katika kipengele cha pizza na tunafanya bidiii ili iwe rahisi kwa wateja wetu kupata pizza zetu bora duniani kote.
Pizza Hut, ambayo ina zaidi ya mighahawa 16,000 duniani kote na kwa mwaka 2015 jumla ya mauzo yake yalikuwa zaidi ya dola za kimarekani bilioni 12, ni kampuni ya mghahawa wa pizza pekee na ya kwanza kuwa katika nchi 100. Pizza Hut iliingia Afrika mwaka 2014 na inaona fursa ya kukua Afrika kwa miaka kadhaa ijayo.
Mkurugenzi wa Dough Works Ltd, Vikram Desai, alishirikisha shauku yake kwa ufunguzi wa mgahawa akisema, “Timu yetu ina furaha na inajivunia kuileta Pizza Hut kwa watanzania. Tumewekeza mamilioni ya dola ili kuendeleza biashara ya Pizza Hut nchini Tanzania na tunampango wa kufungua zaidi ya migahawa minne ya Pizza Hut ifikapo mwishoni mwa mwaka huu. Tunayofuraha kuendelea kuieneza zaidi bidhaa hii ya kimataifa katika jamii yetu, kutengeneza zaidi ya ajira mpya 500 kufikia mwisho wa mwako 2019 na kuendeleza zaidi sekta ya QSR. “
Pizza Hut mpya inapatikana katika maeneo ya Mkuki Mall barabara ya Nyerere jijini Dar Es Salaam. Mgahawa umepambwa kwa mtindo wa kisasa, ubao unaoonyesha aina na bei ya pizza ni wa kidijitali, ina sehemu ya kucheza watoto na ina siti za kukaa watu 90. Bali na ladha ya kimataifa ya Pizza Hut,pia kuna orodha ya menu yenye ladha inayopendwa nchini kama vile Peri-Peri chicken, Paneer Vegorama na Tandoori Paneer pizzas.

0 maoni:

Chapisha Maoni