Alhamisi, 5 Mei 2016

Mwanamke atolewa hai kwenye vifusi Nairobi


Mwanamke ametolewa akiwa hai kutoka kwenye vifusi siku sita baada ya jumba kuporomoka katika mtaa wa Huruma, Nairobi.
Juhudi za uokoaji bado zinaendelea ingawa kuna wasiwasi kwamba muda wa kupata manusura wakiwa hai unayoyoma.

Jengo
Image captionJengo hilo liliporomoka baada ya mvua kubwa kunyesha Ijumaa
Kwa mujibu wa Pius Masai, mkuu wa kitengo cha taifa cha kukabiliana na majanga, idadi ya waliofariki kufikia sasa imefikia 36.
Watu 136 wameokolewa wakiwa hai lakini watu 70 kufikia sasa bado hawajulikani walipo.
Siku mbili zilizopita, mtoto wa umri wa miezi sita aliokolewa baada ya kukaa kwenye vifusi kwa siku nne.
Msichana huyo alitolewa kwenye vifusi mwendo wa saa kumi usiku na kupelekwa hospitalini.
Mwanamke
Image captionMaafisa wa uokoaji bado wanawatafuta manusura zaidi
Alipatikana akiwa amefunikwa kwa blanketi ndani ya ndoo na hakuonekana akiwa na majeraha yoyote.
Babake mtoto huyo, Bw Ralson Wasike, akihutubia wanahabari baadaye, alisema bintiye amekuwa na nguvu sana.
BBC

0 maoni:

Chapisha Maoni