Taasisi ya MasterCard kupitia mfuko wake kwa ajili ya maendeleo vijijni 2015 imetangaza washindi watano wa shindano la ubunifu unaoweza kusaidia kupunguza umaskini na kuongeza upatikanaji wa huduma za kifedha kwa watu maskini waishio vijijini barani Afrika ambao watapatiwa zaidi ya Dola Milioni 10 ili kufanikisha ubunifu wao.
Akizungumzia shindano hilo, Mshauri Ufundi wa MasterCard Foundation, Gabriel Kivuti ameyataja makampuni ambayo yameshinda ni APA Insuarence Ltd, Finserve Africa Ltd, M-KOPA LLC, Musomi Kenya Ltd na Olam Uganda Ltd na Tanzania ikitoa mshindi mmoja ambaye ni M-KOPA LLC.
“Dola Milioni 10 watapatiwa washindi ili waweze kusaidia kupunguza umaskini vijijini kwa Tanzania M—KOPA watatoa vijijini Sola na wataweza kusaidia huduma za utumaji wa fedha kwa kutumia simu ya mkononi,” alisema Kivuti.
DSC_1593
Mshauri Ufundi wa MasterCard Foundation, Gabriel Kivuti akielezea jambo kwa w
Pamoja na kutangaza washindi hao , pia MasterCard imezindua shindano lingine la Mfuko Kwa Ajili ya Maendeleo Vijijini 2016 ambalo lilianza kupokea maombi kwa wanaohitaji kushiriki tangu Aprili, 14 ambapo maombi yatapokelewa hadi Juni, 10.
Kivuti amesema kuwa watapokea maombi kutoka sehemu mbalimballi duniani ili kuona ni jinsi gani kampuni hizo zitaweza kubuni njia mbadala ambazo zinaweza kutumika kupunguza umaskini vijijini katika nchi nane za Afrika ambazo ni Ivory Coast, Tanzania, Ghana, Kenya, Msumbiji, Senegal, Uganda na Zambia.
DSC_1619
Baadhi ya waandishi wa habari na wawakilishi wa taasisi mbalimbali waliohudhuria mkutano huo.