Jumatano, 4 Mei 2016

KUTANA NA ‘GREEN VOICES’, SAUTI ZA AKINAMAMA WAPAMBANAO NA MABADILIKO YA TABIANCHI

Akinamama wanaoshiriki katika mradi wa kupaza sauti za wanawake
wanaopambana na mabdiliko ya tabianchi – Green Vocies katika picha ya pamoja na
viongozi wa Foundation For Women of Africa na wafadhili wa mradi huo, mara
baada ya uzinduzi wa mradi huo Madrid, Spain hivi karibuni.
 Mama Maria Tereza (katikati) – Rais wa taasisi ya Foundation
for Women of Africa akiwa na waandishi wa habari wanaotekelza mradi wa Green
Voices wakati wa hafla ya kuwakaribisha kinamama nchini Spain. Kutoka kushoto ni Secelela Balisidya, Tukuswiga Mwaisumbe, Farida Hamis,
Siddy Mgumia na aliyechuchumaa Judica Losai.
Akinamama wanaoshiriki katika
mradi wa kupaza sauti za wanawake wanaopambana na mabdiliko ya tabianchi –
Green Vocies katika picha ya pamoja na uongozi wa chuo kikuu cha Universitad
Automous De Madrid, mara baada ya kutembelea mazingira ya chuo hicho Madrid,
Spain hivi karibuni.
Ziara ya mafunzo kujifunza
jinsi ya kutengeneza mbolea ya mboji.
Ziara ya mafunzo kujifunza
majiko yanayotumia nishati ya jua.
Ziara ya mafunzo katika chumba
cha habari cha gazeti la El Pais.
Akimama na wawezeshaji wa
mafunzo katika picha ya pamoja darasani.
 …………………………………………………………………………………………………………..
WANAWAKE wapatao 15 hivi karibuni walihudhuria mafunzo ya kuongeza ujuzi wa jinsi ya kupambana na mabadiliko ya tabianchi nchini Spain. Mafunzo na mradi huo vinafadhiliwa na Taasisi inayojihusisha na maendeleo ya wanawake wa Afrika, ijulikanayo kama Foundation for Women of Africa  inayoongozwa na Makamu wa Rais mstaafu waSpain Mama  María Teresa Fernández de laVega.
Taasisi hiyo itafanya kazi na wanawake hao 15 wa kitanzania kupitia miradi inayosaidia nchi kupambana na mabadiliko ya tabianchi. Wanawake hao ambao kati yao watano ni waandishi wa habari kila mmoja atatekeleza mradi mmoja, huku waandishi wa habari wakisaidia kupaza sauti za akinamama hao kupitia vyombo
mbalimbali vya habari nchini.
Mradi huu unaojulikana kama GREEN VOICES una lengo la kupaza sauti za akinamama kueneza ujuzi wao wa kupambana na mabadiliko ya tabianchi ili jamii nzima ya kitanzania iweze kujifunza zaidi na kuzitumia mbinu hizo katika kupambana na mabadiliko ya tabianchi. Mradi huo unaoratibiwa hapa nchini na Mtandao wa wanahabari wa Mazingira (EMNet) kwa niaba ya Foundation for Women of Africa unatekelezwa katika mikoa
sita ya Kigoma, Kilimanjaro, Mwanza, Morogoro, Dar es Salaam na Pwani ukihusisha miradi ya kilimo, usindikaji, ufugaji na utafiti.
Mratibu wa EMNet Secelela Balisidya amesema akinamama hao wanatekeleza miradi ambayo inachangia moja kwa moja aidha kupambana au kupunguza athari za mabadiliko ya tabianchi. Amesema miradi hiyo ni mradi wa kilimo cha miti ya matunda mkoani Kigoma, kilimo cha viazi lishe visiwani Ukerewe mkoani Mwanza, Ufugaji Nyuki mkoani Morogoro na Pwani na ukaushaji wa mbogamboga kwa kutumianishati ya jua mkoani Morogoro.
Miradi mingine ni usindikaji wa vyakula mbalimbali kutokana na muhogo mkoani Pwani, kilimo hai cha mbogamboga na kilimo cha uyoga mkoani Dar es Salaam, mradi wa majiko banifu mkoani Pwani na mradi wa
utafiti wa jiko linalotumia nishati ya jua mkoani Kilimanajro. Mradi huo unaotarajiwa kutelekezwa kwa mwaka mmoja unatoa fursa kwa kinamama kutoa ujuzo wao wa kupambana na mabadiliko ya tabianchi na sauti zao kusikika.

Hiyo ni kwa sabuabu kinamama wana uhusiano mkubwa na mazingira kutokana na kazi wanazozifanya kila siku za kilimo na utunzaji wa familia kuhusiana moja kwa moja na mazingira hivyo kuyaelewa zaidi mazingira na jinsi ya kupambana na mabadiliko ya tabianchi.
Wakiwa Madrid nchini Spain walikopata mafunzo wa wiki mbili katika chuo kikuu cha Autonomus Universitad De Madrid, akinamama hao na waandishi wa habari walijifunza kwa nadharia na vitendo jinsi nchi ya Spain inavyokabiliana na  mabadiliko ya tabianchi na kuona njia ambazo na huku nchini zinaweza kutumika
kupambana na mabadiliko ya tabianchi. Mafunzo kwa vitendo pia yalihusisha ziara za mafunzo kujifunza kilimo hai, na jinsi nishati jua inavyoweza kusaidia kupambana na mabadiliko ya tabianchi.
Waandishi wa habari pia walipata nafasi ya kutembelea chumba cha habari
cha gazeti la Serikali ya Sapin la El Pais an kujifunza zaidi jinsi waandishi wa huko wanavyoandika habari
zihusianazo na mabadiliko ya tabianchi.  


0 maoni:

Chapisha Maoni