Jumanne, 10 Mei 2016

HALMASHAURI YA WILAYA YA IRINGA KUHAMISHA MAKAO YAKE MAKUU





MAKAO Makuu ya Halmashauri ya Wilaya ya Iringa yatahamishwa kutoka Iringa Mjini ambako yako kwa miaka yote tangu ianzishwe na kupelekwa katika moja ya maeneo ya yanayounda halmashauri hiyo.

Halmashauri hiyo yenye zaidi ya wakazi 245,000 kwa mujibu wa sensa ya mwaka 2002, inaundwa na zaidi ya kata 20 zenye majimbo mawili ya uchaguzi, Kalenga na Isimani.

Akitoa taarifa hiyo kwenye kikao cha baraza la madawani la halmashauri hiyo, Mwenyekiti wa halmashauri hiyo, Steven Mhapa alisema makao makuu ya halmashauri hiyo yatajengwa nje ya manispaa ya Iringa ili kusogeza huduma jirani na wananchi.

Pamoja na azma hiyo aliyosema ina baraka zote za serikali, Mhapa alisema halmashauri hiyo iko pia katika mpango wa kujenga hospitali yake ya wilaya wakati ikiendelea kuitumia hospitali teule ya halmashauri ya wilaya hiyo ya Tosamaganga.

“Kazi iliyopo mbele yetu ni kufanya utafiti ili kujua wapi makao makuu ya halmashauri yetu yajengwe,” alisema huku baadhi ya wajumbe wa baraza hilo wakitilia shaka uamuzi huo kutokana na jiografia ya halmashauri hiyo iliyovyo.

Alisema wakikamilisha utafiti huo, kazi ya ujenzi wa makao hayo mapya inaweza kuanza mwaka ujao wa fedha.

“Tukifanikiwa majengo hayo ya halmashauri hapa mjini Iringa, tutayatumia kama moja ya vitega uchumi vya halmashauri yetu,” alisema.

Wakati huo huo, Mhapa alisema halmashauri hiyo imetenga Sh Milioni 120 zitakazotumika kuunga mkono jitihada za wadau wao wa elimu ili kukubaliana na tatizo la madawati katika shule zake.

Maoni 2 :

  1. Je,lea Musa huu uliobaki makao ya halmashauri ya iringa vijijini yatakuwa wapi?

    JibuFuta
  2. Je,Muda huu uliobaki makao ya halmashauri ya iringa vijijini yatakuwa wapi?

    JibuFuta