Jumamosi, 13 Agosti 2016

YANGA YAIBANJUA MO BEJAIA YA ALGERIA KAMOJA UWANJA WA TAIFA

1
Mchezaji wa timu ya Yanga Obrey Chrwa akiwatoka wachezaji wa timu ya Mouloudia  Bejaia ya Argeria kwenye mchezo wa Klabu Bingwa Barani Afrika uliofanyika kwenye uwanja wa Taifa leo huku Yanga ya Tanzania ikiibuka kwa goli  lililofungwa na Mchezaji wa kimataifa kutoka  nchini Burundi, Amisi Tambwe dakika ya tatu ya mchezo dhidi ya Timu ya  Mouloudia  Bejaia ya nchini Algeria.
Baada ya ushindi huo Yanga wanaendea kusalia katika  nafasi ya nne wakiwa na alama nne huku mchezo kati ya Mazembe na Medeama ukitarajiwa kuchezwa kesho nchini Ghana ukisubiriwa ili kuona kama unaweza kuleta msimamo tofauti wa kundi hilo baada ya mchezo huo wa kesho. 
2
Mashambulizi golini mwa timu ya Mouloudia  Bejaia yakiendelea timu ya Yanga ilistahili kushinda magoli mengi lakini washambuliaji wa timu hiyo hawakuwa makini kwani mipira mingi ilipotelea pembeni mwa milingoti ya goli ama ilidakwa na golikipa wa timu hiyo.
4 5
Mashabiki wa timu ya Yanga wakishangilia wakati mchezo huo ukiendelea kwenye uwanja wa Taifa

0 maoni:

Chapisha Maoni