Na Mahmoud Ahmad Arusha
CHAMA Cha wakulima nchini TASO ,kanda ya ksikazini kimepiga
marufuku mabanda ya maonyesho ya wakulima Nane nane yaliyopo viwanja
vya maonyesho vya Taso Themi Hill,jijini Arusha,kugeuzwa matumizi na
kuwa ni ya biashara ya mama lishe na shughuli za ufugaji na kutaka
yabakie kwa ajili ya maonyesho tu.
Hayo yamefikiwa jana kwenye awamu ya pili ya kikao cha
uongozi wa Taso na wadau ambao ni wamiliki wa mabanda kilichohusu
maandalizi yamaonyesho ya wakulima Nane nane mwaka huu na kusisitiza
kuwa Taso haifanyi biashara na hairuhusu wamiliki wa mabanda hayo
kuyageuza na kuwa ni sehemu ya biashara.
Mwenyekiti wa Taso, Ather Kitonga, amesema iwapo Taso
itaruhusu mabanda hayo kubadilishwa matumizi badala ya shughuli za
maonyesho yakatumika kwa ajili ya biashara ,yatakuwa yamepoteza maana
halisi ya mabanda ya maonyesho na Taso haiko tayari kwa hilo.
Amesema shughuli ya biashara zinafanywa na walinzi kwa
ajili ya kujiongezea vipato mara tu maonyesho ya wakulima
yanapomalizika na hiyo inatokana na mawasiliano duni kati ya
halmashauri za wilaya kupitia kwa maafisa kilimo na mifugo ambao huwa
hawatembelei mabanda hayo mara maonyesho yanapomalizika.
Kitonga, amesema kupitia uduni huo wa mawasiliano walinzi
wameyageuza mabanda hayo kuwa ni ya mama lishe, na ufugaji na hivyo
kwenda kinyume na malengo ya viwanja vya maonyesho ya wakulima.
Amesema kuanzia Juni 28 mwaka 2016 ni marufuku kwa
halmashauri za wilaya kugeuza nyumba na mabanda yaliyoko ndani ya
viwanja hivyo kuwa ni makazi ya kudumu na kuyageuza kuwa ni sehemu ya
kufugia mbwa na kuku.
Kitonga, amesema Taso imezitaka halmashauri zote za wilaya
,kuhakikisha zinaondoa mbwa na kuku wanaofugwa kwenye mabanda hayo
sanjari na kuhakiki walinzi wao na nyumba na mabanda ya maonyesho ili
kudhibiti ubadilishaji wa matumizi kwa kuyageuza kuwa ni ya kufugia
mifgo na wanyama .
.Aidha Taso imezitaka halmashauri zote za wilaya
kuhakikisha zinakuwa na takwimu za teknolojia ya kilimo na mifugo ili
kuwasaidia wananchi kubadilisha shughuli zao na kuzifanya ziwe na tija
badala ya kufanya kwa mazoea.
Kitonga, amesema ili teknolojia hizo ziwafikie walengwa
lazima wataalamu wa kilimo waoteshe mbegu za vipando na halmashauri
zijikite kwenye vipando kwa kutoa elimu kwa wakulima namna ya kulima
kibiashara ili wapate faida .
Ameongeza kuwa Taso imejipanga kuhakikisha teknolojia ya
kilimo inawafikia wakulima na maonyesho hayo yanakuwa ni yenye tija na
sio kuwa ya mazoea .
Amesema maonyesho hayo yanaanza rasm I Augosti mosi na
kumalizika Augositi kumi na kuwataka watakaoshiriki kwenye maonyesho
hayo mwaka huu kuzingatia kalenda hiyo ambayo inakusudia kutoa muda
mrefu zaidi kwa waonyeshaji badala ya kumalizika Augoti 8sasa kilele
chake kitakuwa Augosti 10.
Kwa upande wake Katibu mkuu wa Taso kanda ya kasikazini
Jeremiah Sembose, amesema changamoto kubwa iliyopo ni kwenye vipando
ambapo asimia 90% ya mbegu hazina ubora na hivyo vipando vinashindwa
kutoa ujumbe halisi wa shamba darasa kwa wakulima wanaotembelea ili
kujifunza.
Sembose, amesema kuwa tayari Taso, imeshapokea kauli mbiu
ya maonyesho ya mwaka huu kutoka wizara ya kilimo isemayo Kilimo, uvuvi
na mifugo ni nguzo ya maendeleo vijana shiriki kikamilifu hapa kazi tu.
Kuhusu maandalizi ya mabanda ya maonyesho, Sembose, amsema
uongozi wa Taso, mara baada ya kutembelea mabanda hayo haujaridhishwa
na hatua ya maandalizi na imegundua kuna changamoto mbalimbali .
Amezitaja baadhi ya changamoto hizo kuwa ni pamoja na
kutokufikia asilimia 50%,maandalizi kwa halmashauri za wilaya za
Same,Moshi na Ngorongoro zikiongoza kwa kuwa na hali mbaya ya
maandalizi.
Sembose, amesema kutokana na hali hiyo, Taso, imezitaka
halmashauri zote za mikoa ya Arusha, Manyara na Kilimanjaro,
kuhakikisha zinaanza maandalizi ambayo yatahusisha upakaji rangi mabanda
yote, usafi, upandaji wa vipando ikiwa ni shamba darasa ,kuimarisha
miundo mbinu, kubosha mazingira .
0 maoni:
Chapisha Maoni