Kama umekuwa ukitumia huduma za kibenki nchini unaweza usiwe mgeni sana wa ujumbe uliosambazwa na benki mbalimbali nchini kuwa kuanzia Juai, 1 zitakuwa zikikata asilimia 18 ya kodi ya VAT kwa huduma za kifedha wa wateja wa benki hizo.
Jambo hilo lilichukua sura mpya pale ambapo TRA ilipotoa taarifa na kuwa jambo hilo sio sahihi na mabenki ndiyo yanatakiwa kukatwa pesa hiyo tofauti na taarifa waliyotoa ya kutaka kumkata mteja ambaye ndiye mmiliki wa pesa hizo.
Ili kumaliza utofauti uliopo kati ya mabenki, BoT na TRA, Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Phillip Mpango amelitolea jambo hilo ufafanuzi na kueleza kuwa pesa hiyo inatakiwa kukatwa kwa mabenki na sio kwa mtumiaji.
“Kodi hiyo ya aslimia 18 inatakiwa kukatwa kwa benki sio kwa mteja, mabenki haya yamekuwa yakipata pesa nyingi sana bila kutoa pesa hiyo sasa ni muda ambao wanatakiwa kuitoa pesa hiyo sio kuwatupia mzigo wananchi,
“Niwatoe hofu Watanzania wawe na amani serikali inalishughulikia jambo hilo na tutashughulika na mabenki ili kuhakikisha mzigo huo unasalia kuwa wao,” alisema Dk. Mpango.