Jumatatu, 4 Julai 2016

MADAWATI 40 YALIYOTENGENEZWA CHINI YA KIWANGO KWA FEDHA ZA MFUKO WA JIMBO,WILAYANI KILOLO MBUNGE AYAKATAA




Mbunge wa jimbo la kilo Venansi Mwamoto akizungumza na wananchi wa kijiji cha Nyanzwa .Picha na Esta Malibiche
madawati yaliyotengenezwa na kijiji kwa Tsh 20,000 
madawati yaliyochini ya kiwango yaliyotengenezwa na ofisi ya Mbunge ambayo yamechakachuliwa kila moja limechongwa kwa Tsh 50,000
Mbunge wa Kilolo  Mkoani Iringa Venansi Mwamoto amekataa kupokea  madawati 40 yaliyotengenezwa chini ya kiwango,kupitia fedha za mfuko wa jimbo na kisha kukabidhiwa katika kijiji cha Nyanzwa wilayani humo

Akizungumza leo na wananchi wa kijiji cha Nyazwa wilayani humo Mwamoto alisema  
ofisi yake imetoa fedha kwa ajili ya  kutengeneza madawati ili kupunguza kero za madawati katika shule zilizopo wilayani humo,na kuhakikisha wanafunzi wanaondokana na adha ya kurundikana katika dawati moja.
Mbunge huyo alisema  jumla ya Tsh milioni 30 zilitolewa kutoka mfuko wa jimbo kwa ajili ya madawati 600,lakini kati ya madawati hayo ,madawati 40 yametengenezwa chini ya kiwango tofauti na fedha iliyotolewa.

‘’’’’’’Baada ya kukagua madawati hayo yaliyotengenezwa kwa pesa za mfuko wa jimbo ,kuwa sijapendezwa kabisa kwasababu yapo chini ya kiwango na hayana ubora wowote ukulinganisha na fedha zilizotolewa’’’’alisema mwamoto

Mwamoto alisema haiwezekani madawati ya kijiji yaliyotengenezwa kwa Tsh 20,000 yakawa bora zaidi kuliko madawati ya mfuko wa jimbo ambayo yametengenezwa kwa gharama kubwa ya Tsh 50,000 kwa kila dawati.

Hivyo ameutaka uongozi wa serikali ya kijjji hicho kutokubali kupokea madawati hayo ambayo yapo chini ya kiwango kwani hayupo tayari kuona fedha hizo zimechakachuliwa na kuwanufaisha watu badala ya kwenda kwenye lengo husika.

by Esta Malibiche on July 4,2016 in Jamii with No Comment


0 maoni:

Chapisha Maoni