Jumatatu, 4 Julai 2016

JINAMIZI LA MUZIKI WA NGOMA AFRICA BAND KUSUMBUA TENA ULAYA,

indexNa Zainab Ally Hamis
Dar es salaam School of Journalism(DSJ)

Kikosi kazi cha Ngoma Africa Band a.k.a FFU yenye makao yake kule Ujerumani,wanategemewa kukwea majukwaa ya maonyesho Afrika-Karibik, siku ya jumamosi 16 Julai 2016 mjini Bayreuth,Ujerumani pia siku ya 23 Julai 2016 katika tamasha kubwa la International Afrika Festival Tubingen,
siku ya 30 Julai 2016 watatumbuiza XXL Afro Sommer Jam mjini Stuttgart katika Kutur Arena. mzimu huo wa muziki wa bongo dansi utaendelea kudatisha washabiki siku 13 Agosti 2016 mjini Frankfurt katika Afro-Karibik    viwanja vya Robestock Park,Frankfurt,Ujerumani.

Bendi hiyo maarufu ya muziki wa dansi barani ulaya imefanikiwa kuwanasa maelfu washabiki kwa wingi inayoongozwa na mwanamuziki nguli  Ebrahim Makunja. a.k.a kamanda Ras Makunja wa FFU, itapeleka mzimu wake wote wa dansi katika maonyesho hayo makubwa na ya aina yake kwa mashabiki wa muziki katika maonyesho hayo, ambapo  watakumbana “Jino kwa Jino” na makombora ya muziki wa Ngoma Africa band.

Bendi hiyo kwa sasa inatamba nyimbo zake za “Mapenzi ya Pesa” na single CD ya “La Mgambo” pia msikose kusikiliza nyimbo “Supu ya Mawe” ,”Uhuru wa Habari” na “Bongo Tambarare” ambazo zipo katika CD ya “BONGO TAMBARARE” zote zinasikika katika kambi ya FFU au web yao

0 maoni:

Chapisha Maoni