Waziri
wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu
akiongea na Wajumbe wa Mkutano wa Viongozi Wanawake katika masuala ya
Afya katika Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa Jijini Dar es Salaam 5 Mei,
2016.
Balozi
wa Denmark nchini Tanzania, Mhe. Einar Hebogard Jensen akiongea na
Wajumbe wa Mkutano wa Viongozi Wanawake katika masuala ya Afya katika
Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa Jijini Dar es Salaam, 5 Mei, 2016.
Balozi
wa Denmark nchini Tanzania, Mhe. Einar Hebogard Jensen akiongea na
Wajumbe wa Mkutano wa Viongozi Wanawake katika masuala ya Afya katika
Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa Jijini Dar es Salaam, 5 Mei, 2016.
Waziri
wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu
(kushoto) pamoja na Balozi wa Denmark nchini Tanzania, Mhe. Einar
Hebogard Jensen wakifurahia burudai toka kwa Vijana wakiotumbuiza
stejini (hawapo pichani) wkaati wa Mkutano wa Viongozi Wanawake katika
masuala ya Afya uliofanyika Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa Jijini Dar es
Salaam 5 Mei, 2016.
PICHA ZOTE NA BENEDICT LIWENGA-MAELEZO.
………………………………………………………………………………………………………………………….
Na Jonas Kamaleki- MAELEZO.
Wizara ya Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto inakusudia kutoa taarifa ya wanawake
wanaofariki Dunia kutokana na matatizo ya uzazi kila baada ya miezi
mitatu ili kukabiliana na tatizo la vifo vya wanawake nchini.
Hayo yamesemwa na Waziri wa
Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu leo
jijini Dar es Salaam wakati akifungua Mkutano wa Viongozi Wanawake
katika masuala ya Afya.
“Nimeamua kuhakikisha wanawake
wanapiga hatua na kuthaminiwa katika jamii, na nimeamua kuanza kutoa
ripoti ya robo mwaka kwa kila Halmashauri kuhusu taarifa ya wanawake
wanaofariki kutokana na matatizo ya uzazi,” alisema Ummy Mwalimu.
Ameeleza kuwa, katika uteuzi
atakaoufanya kwenye bodi zilizo chini ya Wizara yake, atahakikisha
asilimia 30 ya wajumbe wa bodi hizo ni wanawake. Baadhi ya Bodi zilizo
chini ya Wizara yake ni pamoja MSD, TFDA na Bodi ya Wafamasia.
Aidha, Mhe. Ummy amemshukuru
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli
kwa kutekeleza sera ya elimu bure ambapo amesema wazazi watalazimika
kuwapeleka watoto wa kike shuleni kwa wingi kuliko ilivyokuwa awali.
Katika kutilia mkazo suala la
elimu kwa wasichana, Waziri Ummy amasema watoto wa kike hawana budi
kujitambua na kuzingatia masomo ambayo ndiyo yatawafanya waweze
kuchagulika au kuteuliwa kushika nyadhifa kubwa za uongozi. “Hamsini kwa
Hamsini bila elimu ni siasa tu” alisisitiza Mhe. Waziri.
Mhe. Ummy amewataka wanawake
kujituma katika kufanya kazi ili kuibadilisha jamii. Hapa akaja na kauli
mbiu kuwa “Mwanamke akitenda, jamii itatenda, Tanzania Itasonga
mbele’’.
Kwa upande wake Mwenyekiti
Mtendaji wa Tume ya Taifa ya Kudhibiti Ukimwi (TACAIDS), Bibi Fatuma
Mrisho amewasisitiza watoto wa kike kuthamini masomo na kuepuka ndoa za
utotoni. Amesema kuwa mtoto anapokuwa shuleni anaepuka Ukimwi kwa
asilimia saba. Hivyo amesema ni lazima wasichana kupenda shule na kuacha
kurubuniwa na wavulana.
Huu ni mkutano wa utangulizi
kabla ya mkutano Mkubwa wa karne kuhusu Afya, Haki na Ustawi wa
Wasichana na wanawake ambao wajumbe zaidi ya 5,000 wakiwemo viongozi wa
Dunia, Wasomi, Watunga sera, Wanaharakati, Watu wa habari, dini, Vyama
vya kijamii na Wawakilishi wa sekta binafsi watashiriki.
0 maoni:
Chapisha Maoni