Jumatatu, 16 Mei 2016

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI KUTOKA JESHI LA POLISI MKOA WA MWANZA

msa1KATIKA MISAKO INAYOENDELEA YA KUSAKA NA KUKAMATA WAHALIFU JIJINI MWANZA JESHI LA POLISI LIMEWAKAMATA WATU WAWILI AMBAO NI CHACHA MWITA MIAKA 34 NA RASHIDI MOHAMED MIAKA 33 WOTE WAKAZI WA KITANGIRI WAKIWA NA BHANGI MISOKOTO SITA (6) KITENDO AMBACHO NI KINYUME NA SHERIA ZA NCHI ZINAVYOELEKEZA. MSAKO HUO UMEFANYIKA MNAMO TAREHE 14.05.2016 MAJIRA YA SAA 14.05HRS KATIKA KATA YA KITANGIRI WILAYA YA ILEMELA JIJI NA MKOA WA MWANZA.
ASKARI POLISI WAKIWA KWENYE DORIA WALIWEZA KUFANIKIWA KUPATA TAARIFA ZA WATU HAO, AMBAO WALIKAMATWA NA SASA WAPO KITUO CHA POLISI KWA MAHOJIANO KWA AJILI YA KUWEZA KUPATA TAARIFA ZA WATU WENGINE ZAIDI WANAOJIHUSISHA NA BIASHARA HIYO HARAMU. PINDI UCHUNGUZI UKIKAMILIKA WATAFIKISHWA MAHAKAMANI.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MWANZA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED MSANGI AMESEMA  “KUTOKANA NA KUONGEZEKA KWA VITENDO VYA UHALIFU WA AINA HIYO HAPA MKOANI MWANZA JESHI LA POLISI LINAFANYA MISAKO ENDELEVU YA KUSAKA NA KUKAMATA WAHALIFU KATIKA SEHEMU ZOTE”, HIVYO TUNAOMBA USHIRIKIANO NA WANANCHI WENYE TAARIFA ZA WATU WANAO JIHUSISHA NA BIASHARA HIYO ILI TUWEZE KUWAKAMATA.
KATIKA TUKIO LA PILI
MWENDESHA PIKIPIKI MMOJA ASIYEFAHAMIKA JINA WALA MAKAZI AMEFARIKI DUNIA NA MWENGINE KUJERUHIWA VIBAYA ALIJULIKANA  KWA JINA LA STANLEY MAIMU MIAKA 24 MKAZI WA MABATINI  BAADA YA  PIKIPIKI ZAO KUGONGANA.
AJALI HIYO IMETOKEA MNAMO TAREHE 15.05.2016 MAJIRA YA SAA 15:30HRS KATIKA BARABARA YA NYERERE ENEO LA MABATINI SINAI WILAYA YA NYAMAGANA MKOA WA MWANZA AMBAPO PIKIPIKI NAMBA T.451 BBR AINA YA SANYA IKIENDESHWA NA STANLEY MAIMU ILIGONGANA NA PIKIPIKI NAMBA T.580 CBY AINA YA SANLG AMBAPO MTU ALIYEKUWA AKIIENDESHA PIKIPIKI HIYO ALIFARIKI PAPO HAPO NA KUPELEKEA KUSHINDWA KUFAHAMIKA JINA LAKE PAMOJA NA MAKAZI.
CHANZO CHA AJALI NI MWENDO KASI KWA WAENDESHA PIKIPIKI WOTE WAWILI, MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA HOSPITALI YA RUFAA YA BUAGANDO NA MAJERUHI AMELAZWA HOSPITALI YA RUFAA YA BUGANDO KWA MATIBABU LAKINI HALI YAKE BADO SIO NZURI.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MWANZA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED MSANGI AMETOA WITO KWA WATUMIAJI WA VYOMBO VYA MOTO HASWA WAENDESHA PIKIPIKI (BODABODA) KUZINGATIA ALAMA NA SHERIA ZA USALA BARABARANI ILIKUWEZA KUZUI AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA.
IMESAINIWA NA:
SACP: AHMED MSANGI
KAMANDA WA POLISI (M) MWANZA

0 maoni:

Chapisha Maoni