Waziri
wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu
(kushoto) pamoja na Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Sheria na Katiba,
Mhe. Najma Giga wakielekea Bungeni kwa ajili ya vikao vya asubuhi vya
Bunge hilo leo 16 Mei, 2016 mjini Dodoma..
Waziri
wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Nape Nnauye (kulia) pamoja
na Mbunge wa Viti Maalul CCM, Mhe. Halima Bulembo wakielekea Bungeni
kwa jili ya vikao vya asubuhi vya Bunge hilo leo 16 Mei, 2016 mjini
Dodoma.
Waziri
wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Mhe. Profesa Joyce Ndalichako
(kulia) pamoja na Naibu Waziri, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano, Mhe. Mhandisi Edwin Amandus Ngonyani wakielekea Bungeni kwa
ajili ya vikao vya asubuhi vya Bunge hilo leo 16 Mei, 2016 mjini
Dodoma.
Baadhi
ya Viongozi wa Jeshi la Polisi, Magereza, Uhamiaji na Zimamoto
wakiingia ndani ya Ukumbi wa Bunge mjini Dodoma kwa ajili ya vikao vya
bunge hususan kusikiliza Bajeti ya Wizara ya Mambo y Ndani ya Nchi 16
Mei, 2016 mjini Dodoma.
PICHA ZOTE NA BENEDICT LIWENGA-MAELEZO, DODOMA.
JAMII YAASWA NA KUTAKIWA KUJENGA FAMILIA IMARA
Dar es salaam.
Jamii nchini imeaswa kuendelea
kujenga familia imara kwa kuwa ndicho kitovu cha mabadiliko katika jamii
na maendeleo ya kiuchumi.
Aidha, imekumbushwa kuwa
masuala mbalimbali hujadiliwa, kupangwa na kutekelezwa kuanzia ngazi ya
familia kwa ajili ya kuimarisha ushiriki thabiti wa jamii katika
maendeleo ya taifa.
Hayo yamo katika taarifa
iliyotolewa na Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii ,Jinsia, Wazee na
Watoto wakati wa maadhimisho ya Siku ya familia iliyofanyika Mei, 15,
2016.
Taarifa hiyo imeeleza kuwa
Tanzania iliadhimisha siku hiyo chini ya kauli mbiu ya isemayo “Familia
Yenye Afya Bora ni Mwanga wa Maendeleo”
Taarifa hiyo imebainisha kuwa familia
ni kitovu cha Maendeleo katika jamii hivyo haina budi kutambua kuwa
uzingatiaji wa masuala ya maendeleo ya kijamii na kiuchumi hupaswa
kujadiliwa, kupangwa na kutekelezwa kuanzia ngazi ya familia kwa ajili
ya kuimarisha ushiriki thabiti wa jamii katika maendeleo ya taifa.
Imebainisha kuwa maendeleo ya
nchi hayawezi kufikiwa kama familia hazitakuwa na afya bora hivyo kauli
mbiu ya mwaka huu inalenga kuchochea mafanikio ya malengo ya Maendeleo
Endelevu yatakayozingatia uboreshaji wa huduma ya afya bora ya familia,
malezi bora ya watoto na utunzaji wa afya ya watu wenye mahitaji maalum
wakiwemo wazee na watu wenye ulemavu.
“ Kila mwanafamilia anahitajika
kushiriki katika maadhimisho ya siku hii muhimu kwa kufanya shughuli
mbalimbali za kimaendeleo, ikiwemo vyombo vya habari kuelimisha
wananchi kuhusu umuhimu wa maadhimisho haya ili kuharakisha uboreshaji
wa afya za wanafamilia wote katika nchi yetu” imeeleza sehemu taarifa
hiyo.
Katika hatua nyingine
Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Jinsia Nchini (TGNP) Bi. Lilian Liundi
akiizungumzia siku hiyo katika mahojiano maalum na Idhaa ya Kiswahili
ya Sauti ya Ujerumani (DW) ameeleza kuwa hali ya familia katika maeneo
mbalimbali haiko salama kutokana na changamoto za kiuchumi.
Ameeleza kuwa kumekuwa na
changamoto ya tatizo la mimba za utotoni kwa watoto wa kike na wanawake
kuachiwa familia hivyo misingi ya familia inakuwa siyo bora kutokana na
kuwepo kwa malezi ya upande mmoja.
Naye mchambuzi wa Masuala ya
Siasa kutoka nchini Kenya Bw. Bobby Mkangi ameeleza kuwa kufuatia hali
ngumu ya uchumi misingi ya familia imevurugika na hivyo kupelekea kuwepo
na ajira za watoto ambao badala ya kuwa shule wanafanya kazi ndogondogo
kusaidia kipato cha familia.
Siku ya Familia Duniani
huadhimishwa na nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa kwa mujibu wa Tamko
la Baraza la Umoja wa Mataifa namba 47/257 la Septemba 20, 1993.
0 maoni:
Chapisha Maoni