Jumatano, 11 Mei 2016

SERIKALI KUKAMISHA MAABARA NNE ZA UPIMAJI KIFUA KIKUU NCHINI.


Na Tigaya Vincent_MAELEZO-Dodomaimages
Wizara ya Afya , Maendeleo ya Jamii ,Jinsia Wazee na Watoto ipo katika hatua za mwisho za kukamilisha maabara nne za Kanda ili kuboresha huduma za vipimo vya upimaji wa kifuu na kifuaa kikuu sugu.
 
Hatua hiyo inalenga kuimarisha na kusogeza huduma karibu za upimaji wa kifuaa  kwa wananchi.
 
Kauli hiyo imetolewa leo mjini Dodoma na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia , Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu wakati akiwasilisha Bungeni hotuba kuhusu makadirio ya mapato na matumizi ya fedha kwa mwaka ujao wa fedha 2016/17.
 
Amezitaja hospitali hiso ambazo zitakuwa na maabara hizo kuwa ni Hospitali ya Rufaa ya Mbeya, Hospitali ya Rufaa ya Bugando, Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma na Hospitali ya Kibong’oto mkoani Kilimanjaro.
 
Waziri Ummy aliongeza kuwa Wizara hiyo itaendelea matibabu ya kifua kikuu sugu katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili na Hospitali ya Bugando.
 
Aidha ,Waziri huyo aliongeza kuwa Wizara imefanikiwa kufikia idadi ya vituo 547 vinavyotoa huduma shirikishi za kifua kikuu na UKIMWI nchini .
 
Hatua hii inalenga kuondoa usumbufu kwa wagonjwa wenye maambukizi mseto ya Kifuua Kikuu na UKIMWI kupata huduma sehemu moja.
 
Waziri Ummy aliongeza kuwa chini ya utaratibu huo , Wizara imefanikiwa kutoa huduma  watu 692,642  wanaoishi na Virusi vinavyosababisha UKIMWI (WAVIU)  ili kubainisha uwepo na kutokuwepo kwa maambukizi ya kifua kikuumiongoni mwao.
 
Alisema kuwa kati ya hao watu 26,218 waligundulika kuwa na maambukizi ya kifua kikuu na walipatiwa matibabu.
 
Aidha  , Waziri huyo alisema kuwa katika mwaka ujao wa fedha ,Wizara hiyo itaendelea kutoa huduma za matibabu ya kifua kikuu sugu kufikia hospitali kumi za mikoa ya Dar es salaam, Mbeya, Mwanza, Dodoma, Morogoro, Mtwara, Tanga, Shinyanga, Geita na Mara.
 
Alisema kuwa Wizara itaongeza  uwezo mikoa 16 yenye viwango vya chini kabisa vya uibuaji wagonjwa wa kifua kikuu ili kuongeza kasi ya kudhibiti ugonjwa huo nchini.
 
Katika mwaka  ujao wa fedha Wizara hiyo iliomba Bunge  likubali kuidhinisha makadirio ya matumizi ya Wizara pamoja na Taasisi zake yenye jumla ys shilingi 845,112,920,056.00.
 
Kati ya  fedha hizo  shilingi 317,752,653,000.00 ni kwa ajili ya matumizi ya kawaida na shilingi 527,360,267,056.00 ni kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo.

0 maoni:

Chapisha Maoni