Na Benedict Liwenga (Maelezo)
…………………………………….
Katika Dunia tuishiyo sasa binadamu hatuko peke yetu, lakini tumejijengea dhana kuwa tunaishi peke yetu huku tukisahau kuwa Mungu kaumba viumbe kadha wa kadha vinavyoonekana na visivyoonekana.
Unaweza
kushangaa ama kudhani kuwa namaanisha juu ya uwepo wa nguvu za kigiza,
La Hasha!, mtu anapokuuliza kwamba Je unafahamu maana ya neno ‘UFO’ (Unidentified Flying Object)? Bila shaka watu wengi watakuwa hawafahamu kuhusiana na vitu hivi na wengine wanaweza kukupa maana nyingine tofauti na mada.
Neno
UFO limechukua kasi kwenye vyombo vya habari vingi duniani hasa vya
wenzetu wa nchi za Magharibi, pia upande wa Asia ambapo baadhi ya
Wataalam wamajaribu kufuatilia kwa karibu juu ya vitu hivi na wapi
vimetokea na madhumuni ya kuonekana ovyo katika maeneo tofauti na
madhara yake lakini hakuna maelezo mazuri yanayoweza kuelezeka katika
hilo, na hii imepelekea wataalam hao kuziita baadhi ya tafiti zao kuwa
ni zisizoelezeka (Unexplained files about UFOs)
Ebu tujiulize maswali UFOs ni vitu gani, na malengo yake kuonekana duniani ni nini haswa?
UFOs
ni Vyombo vyenye ukubwa tofauti na maumbile tofauti ambapo vingine
vinakadiliwa kuwa na ukubwa wa futi 100 ama zaidi vingine na muonekano
wake ni wa duara kama sahani kubwa la chuma lenye kung’aa (steel
shaped-saucer), lakini pia vinaweza kuwa na umbo mengine tofauti kama
vile maumbile ya pembe tatu ambapo kwa chini zinakuwa ya na taa zenye
kutoa miale mikali ya mwanga yenye rangi ya bluu, nyekundu na nyeupe.
Continue reading →
0 maoni:
Chapisha Maoni