Jumapili, 1 Mei 2016

Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Iringa, Rose Tweve AKUTANA NA WALEMAVU WA MACHO

B1 Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Iringa, Rose Tweve (kushoto) akisalimiana na mkazi wa Iringa mjini, Rebeca Mkwavi ambaye ni mlemavu wa macho jana alipokutana nao katika ofisi za Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Iringa mjini, mbunge huyo alitoa msaada wa Sh 1 milioni kwa wanawake walemavu 20  kwa ajili ya kuanzisha miradi ya kiujasiriamali. picha na Mpigapicha Wetu. B3Mkazi wa Iringa Mjini ambaye ni mlemavu wa macho Anna Kaheya (kulia) akipokea  kitita cha Sh 1milioni kutoka kwa Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Iringa, Rose Tweve (kushoto) jana kwa niaba ya wanawake wenzake 20 wenye ulemavu kwa ajili ya kuanzisha miradi ya ujasiriamali. Mbunge huyo alikutana na wanawake hao Ofisi za Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Iringa mjini zilizopo Sabasaba.  Picha na Mpigapicha Wetu
B2Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Iringa, Rose Tweve (katikati) akifuhia jambo na wanawake wa Baraza la Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi (UWT) Wilaya ya Iringa Mjini  baada ya kumaliza mkutano wake na wanawake hao kwa lengo la kujiwekea mikakati ya kukuza ujasiriamali kupitia Saccoss ya UWT. Picha na Mpigapicha Wetu.
Picha na mpiga picha wetu

0 maoni:

Chapisha Maoni