…………………………………………
Kiongozi wa
Chama cha Kisoshalisti kilichojulikana kama “NAZI” Adolf Hitler
(1889-1945) alikuwa mmoja kati ya Madikteta dhalimu na mwenye nguvu
kuwahi kutokea katika karne ya 20.
Baada
ya Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia mbabe huyo aliamka kwa nguvu kupitia
Chama hiko cha Wafanyakazi wa Ujerumani na kuchukua udhibiti wa Serikali
ya Ujerumani mnamo mwaka 1933.
Hitler
aliamuru uanzishwaji wa kambi za mateso dhidi ya Wayahudi na makundi ya
watu wengine huku akiamini kuwa kufanya hivyo ilikuwa
chachu na tishio tosha dhidi ya ukuu wa himaya ya Aryani na hatimaye
kusababisha vifo vya zaidi ya Wayahudi wapatao milioni Sita.
Mashambulizi
ya Ujerumani dhidi ya nchi ya Poland mwaka 1939 ndiyo yaliyoanzisha
Vita Kuu ya Pili ya Dunia ambapo mpaka kufikia mwaka 1941Ujerumani
iliteka sehemu kubwa ya ardhi ya Ulaya na Afrika Kaskazini.
Ili
kuepuka kukamatwa kwa kukwepa utumishi katika jeshi la
Austria-Hungary, Adolf Hitler aliondoka toka Vienna na kuelekea Munich
mnamo Mei 1913 lakinibaadaye alilazimika kurudi tena.
Taarifa
za kihistoria zinasema kuwa Kiongozi huyo wa Nazi alijiunga na jeshi la
Bavaria na kuanza kufanya kazi za kujitolea ambapo mwaka uliofuata
alishiriki kikamilifu katika vita ya Kwanza ya Dunia akiwa mstari wa
mbele upande wa Magharibi ambapo uzoefu wake katika vita na mapambano
uliathiri mawazo, fikra na mitazamo yake yote baada ya hapo.
Baada
ya Vita Kuu ya kwanza ya Dunia, Hitler alichukua udhibiti wa chama hiko
cha wafanyakazi wa Ujerumani kama kiongozi hivyo alitumaini
kingemwezesha kushika dola ya Ujerumani punde si punde.
Aliposhindwa
kwenye jaribio la Mapinduzi la mwaka 1923 yeye na wenzake walikamatwa
na kufungwa jela na baada ya kutoka jela alijitahidi kukijenga chama
hiko na kuanza mikakati ya kukamata dola kwa njia zilizo halali.
Hitler
alikusudia kufanya mageuzi na kuendesha sera za kibaguzi ambazo
zingetoa nafasi ya kutosha kwa Wajerumani kuweza kuishi katika himaya
kubwa duniani.
Continue reading →
0 maoni:
Chapisha Maoni