Serikali
imepongeza taasisi isiyo ya Kiserikali ya Makumbusho Urithi Tanga kwa
jitihada nzuri walizofanya za kuandaa makumbusho itakayo hifadhi
utamaduni wa wakazi wa Mkoa wa Tanga.
Pongezi
hizo zimetolewa leo jijini Tanga na Naibu Waziri wa
Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo alipotembelea Makumbusho hayo ya
Urithi Tanga alipokuwa katika ziara yake ya kikazi mkoani hapo
iliyolenga kujua uendeshwaji wa shughuli za kisekta.
“Kazi
hii ya ukusanyaji wa taarifa mbalimbali za wakazi wa Tanga kuanzia
ngazi ya Makabila yote saba ya Mkoa wa Tanga,Mila na Desturi zao, pamoja
na kuhimiza ukarabati majengo ya kale kweli mnahitaji pongezi kwa
uzalendo huo”,
“Serikali
ya China iliahidi kusaidia kujenga Majumba ya Makumbusho kwa nchi za
Afrika hivyo andikeni barua ya Wizarani kuwa ajili ya kuendeleza
makumbusho haya halafu tutaiwasilisha Ubalozi wa China,” alisema Naibu
Waziri Wambura,
Kwa
upande Mkurugenzi wa Makumbusho ya Urithi Tanga Mhandisi Godwin Mhando
alisema lengo la kuanzisha makumbusho hayo ilikuwa ni kutaka kutunza
historia ya Mkoa wa Tanga pamoja na kulinda kuhifadhi Mila na Desturi za
watu wa Tanga kwa ajili ya vizazi vijavyo kwani Mkoa huo unahistoria
kubwa katika nchi.
“Makumbusho
haya ya Urithi Tanga siyo kwa maslahi binafsi bali kwa wanatanga wote
na tumeamua kufanya uhifadhi huu kwa kuwa tumeona ipo haja ya kuhifadhi
historia Mkoa wetu.”alisema Mhandisi Mhando.
Naye
Mkuu wa Wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa alisema ofisi yake itajitahidi
kushirikiana na viongozi wa makumbusho hayo kwa kuhakikisha inafikia
malengo iliyojiwekea kwa maslahi ya wakazi wa Tanga pamoja na Watanzania
wote kwa ujumla.
Aidha
Mkurugenzi huyo wa makumbusho aliendelea kusema kupitia ofisi hiyo
wamekuwa wakipanga siku ambayo hufanya maonesho ya shughuli za
kiutamaduni kama matibabu ya kiasili,kuwepo kwa vyakula vya asili hii
ikiwa ni siku ya maadhimisho ya kuenzi utamaduni wa wakazi wa Tanga.
Hata
hivyo kila Mtanzania ametakiwa kujali asili yake pamoja utamaduni wake
na pia kuenzi kwani ni urithi mkubwa kwa vizazi vijavyo.
0 maoni:
Chapisha Maoni