Mkuu
wa Mkoa wa Manyara, Dk Joel Bendera akizungumza wakati wa tukio hilo la
uzinduzi wa huduma za CHF iliyoboreshwa (ICHF) iliyofanyika Wilayani
Babati, Mkoani Manyara
Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dk.
Hamisi Kigwangalla akihutubia wakati wa uzinduzi wa huduma za CHF
iliyoboreshwa (ICHF) iliyoratibiwa na Shirika la Kimataifa la PHARMA
ACCESS. Tukio hilo limefanyika mapema leo Julai 11.2016, Wilayani Babati
katika mji wa Bashnet.
Baadhi
ya watendaji wa Serikali katika Miji na Vijiji pamoja na maafisa Ustawi
wa jamii wakiwa mbele baada ya Dk. Kigwangalla kuwaita mbele haapo na
kisha kuwapa angalizo la miezi sita wawe wamesimamia vizuri mradi huo
Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dk.
Hamisi Kigwangalla akimkabidhi mmoja wa waancho kadi maalum ya CHF
iliyoboreshwa ambayo alijiunga papo hapo wakati wa tukio hilo la
uzinduzi.
Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dk.
Hamisi Kigwangalla akikagua pikipiki ambazo zilitolewa kwa watendaji
watakaosimamia mpango huo wa CHF iliyoboreshwa
Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dk.
Hamisi Kigwangalla aki-test' moja ya Pikipiki ambazo alizitoa kwa
watendaji watakaokuwa wakisimamia mradi huo. pikipiki hizo zimetolewa na
Shirika hilo la Kimataifa la PHARM ACCESS
Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dk.
Hamisi Kigwangalla akimkabidhi mmoja wa watendaji watakaokuwa
wakiendesha huduma hizo kwa kutumia pikipiki
Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dk.
Hamisi Kigwangalla akikabidhi Ipad maalum kwa ajili ya kutumika kwenye
tukio hilo la CHF iliyoboreshwa
Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dk.
Hamisi Kigwangalla alipata wasaha pia wa kujumuika katika huduma ya
matibabu iliyokuwa ikitolewa bure katika tukio hilo la uzinduzi wa
huduma za CHF iliyoboreshwa
Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dk.
Hamisi Kigwangalla pamoja na wageni wengine akiwemo Mkuu wa Mkoa wa
Manyara wakiwasilia kwenye uwanja huo.
Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dk.
Hamisi Kigwangalla mapema leo Julai 11.2016 amezindua rasmi huduma za
Afya za CHF iliyoboreshwa katika Wilaya ya Babati, Mkoani Manyara ambapo
amewaagiza watendaji wa Serikali wakiwemo Maafisa wa Ustawi wa Jamii,
Walimu,
Watendaji wa Serikali Kata, vijiji na Maafisa Maendeleo kuhakikisha
wanasimamia zoezi la kuhamasisha wananchi wanachangamkia furza za
kujiunga na mfuko huo haraka katika kuboresha afya za wananchi wote.
Dk.
Kigwangalla ambaye alikuwa mgeni rasmi, amesema hayo katika Mji wa
Bashnet ambao upo katika Wilaya hiyo ya Babati, Mkoani hapa.
“Natoa
maagizo kwa watendaji wote kuhakikisha munausaidia kutoa taarifa sahihi
ili wananchi wapate kujiunga na huduma hii ya ICHF. Na pia sitaki
kusikia kama wananchi waliojiunga na hudua hii ya CHF iliyoboreshwa
wanakosa dawa ama huduma huko Mahospitali ama kituo chochote cha Afya,
ikibainika Serikali itachukua hatua kali.
Aidha.
Watendaji wote wakiwemo muliopo kwa jamii huko, muhakikishe
munahamasisha na kuwaingiza wananchi wote kwenye mfuko huu. Natoa miezi
sita kwa Maafisa wa Ustawi wa Jamii, Maafisa Maendeleo, Watendaji wa
Serikali za Vijiji, na Maafisa wengine wote nitakaporejea hapa baada ya
miezi sita nikute huduma hii ya CHF iliyoboreshwa imekuwa kubwa na
wananchi wengi wamejiunga na endapo kwenye eneo lako limekuwa la mwisho
basi hatua kali zitachukuliwa dhidi yako” alieleza Dk. Kigwangalla.
Katika
tukio hilo, lililofanyika katika viwanja vya minada vya Bashnet-Babati,
Dk. Kigwangalla alipata wasaha wa kukabidhi vitendea kazi ikiwemo
Pikipiki kadhaa kwa watendaji ambao watakuwa wakitoa huduma hizo za CHF
iliyoboreshwa, ambapo pia alikabidhi kadi kwa wanachama waliojiunga papo
hapo.
Katika
shughuli hizo ambazo zimeratibiwa na Shirika la Kimataifa la PHARMA
ACCESS, pia Dk. Kigwangalla aliweza kuzindua kituo cha Afya
kilichofanyiwa ukarabati mkubwa na shirika hilo katika kituo cha Afya
cha Dongobesh.
Mbali
na kuzindua kituo hicho cha Afya cha Dongobesh kilichofanyiwa ukarabati
mkubwa na PHARMA ACCESS, Dk. Kigwangalla pia aliweza kuweka jiwe la
msingi katika jengo la chumba cha upasuaji wa kituo hicho ambapo alitoa
miezi sita kwa Afisa Tawala wa Wilaya kuhakikisha wanakamilisha jengo
hilo la chumba cha upasuaji.
0 maoni:
Chapisha Maoni