Serikali
imeagiza Maafisa Habari,Utamaduni ,Sanaa na Michezo Mikoani kuanza
kushirikishwa katika vikao vya maamuzi ili wapate kujua mikakati ya
maendeleo kwa sekta zao.
Agizo
hilo limetolewa na Mheshimiwa Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni Sanaa na
Michezo Annastazia Wambura alipokuwa katika ziara ya kikazi Jijini
Tanga kwa ambapo lengo la ziara hiyo ilikuwa ni kufuatilia utekelezaji
wa shughuli za kisekta kwa Wizara yake katika Mkoa huo.
Mheshiwa
Naibu Waziri Wambura alisema kushirikishwa katika vikao vya maamuzi kwa
watendaji wa Kada hizo kutasaidia kuongeza chachu ya ukua wa sekta hizo
katika mikoa pamoja na kutoa maoni ya kitaalum kwa sekta hizo kutoka
kwao.
“Katika
bajeti ya mwaka wa fedha 2017/2018 mtenge bajeti ya Kitengo cha Habari
na pia mfanye utaratibu wa kupata Maafisa Habari kwa kuanzia ngazi ya
Mkoa,Wilaya ,Halmashauri,pamoja na Jiji kwani kada hii ni muhimu kuwepo
kwa lengo lakusaidia kutangaza maendeleo na fursa zilizopo katika Mkoa
wenu,” alisema Mhe .Wambura.
Pamoja
na hayo Mhe. Naibu Waziri Wambura aliendelea kusema Serikali inataka
wananchi wapate kujua shughuli zote za maendeleo katika Mkoa wao
zinafanyika vipi na mikakati ya maendeleo iko vipo,hivyo ni muhimu
kupata Maafisa Habari watakao wasaidia kufanikisha hilo kazi ya kutoa
habari hizo kwa umma.
Aidha,
Naibu Waziri huyo alisisitiza kuwa Wizara kwa sasa ipo katika
mazungumzo na TAMISEMI kwa jili ya kubadili mfumo na kuanzisha Kurugenzi
za kisekta kwa Maafisa Habari,Maafisa Utamaduni,Maafisa Sanaa na
Maafisa Michezo katika ngazi za Mikoa lengo ikiwa ni kuimarisha sekta
hizo.
Kwa
upande wa Mkuu wa Mkoa wa Tanga Bw. Martin Shigela alisema Mkoa huo
unakabiliwa pia na uhaba wa Maafisa Michezo ,Maafisa Utamaduni na
Maafisa Sanaa katika Mkoa na Halmashauri lakini suala hilo tayari
wameanza kulifanyia kazi kwa kufanya utaratibu wa kupata Maafisa hao.
Halikadhalika
naye Mkuu wa Wilaya ya Tanga Mjini Bw. Thobias Mwilapwa alimshukuru
Mheshimiwa Naibu Waziri kwa ziara yake kwa kuwa ametoa somo zuri la
utendaji na pia anaamini atafanyia kazi kilio cha wadau wa michezo wa
mkoa huo kwani ni mmoja wapo katika historia ya Michezo ,pamoja na
Muziki wa Mwambao (Taarabu) pamoja na Mchezo wa Mbio za Baiskeli.
Pamoja
na hayo naibu waziri huyo alitoa wito kwa wakazi wa Tanga katika
kipindi wanapokuwa wakifanya shughuli za kimila na desturi kama za Jando
na Unyago basi wawashirikishe wataalam wa Afya pamoja na wa Elimu kwa
lengo la kutoa elimu ya afya ya uzazi halikadhalika kuelezewa umuhimu wa
elimu katika maisha ya vijana wanaofanyiwa shughuli hizo.
Hata
hivyo wakazi wote wa mkoa wa Tanga wametakiwa kuongeza juhudi za
kusimamia muenendo mzuri wa maadili ya kitanzania ikiwa ni jukumu la
kila mtu pamoja na kufanya kazi kwa kujituma zaidi kama kauli mbiu ya
Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya HAPAKAZI TU!
0 maoni:
Chapisha Maoni