Wahitimu
wa mafunzo ya ujasiriamali wakiwa katika picha ya pamoja katika mafunzo
yaliyofanyika mkoani Kilimanjaro hivi karibuni na kuwahusisha wenye
mabaa na mameneja wao
Wahitimu
wa mafunzo ya ujasiriamali wakiwa katika picha ya pamoja katika mafunzo
yaliyofanyika mkoani Kilimanjaro hivi karibuni na kuwahusisha wenye
mabaa na mameneja wao
………………………………………………………………………………………………………………………….
-Wenye mabaa,maduka ya vinywaji na mameneja wao waupongeza
Mpango wa kuendeleza
wafanyabiashara wadogo wanaouza bidhaa za kampuni ya TBL Group
ujulikanao kitaalamu kama Retail Development Programme umewanufaisha
ambapo idadi yao hivi sasa wanaendesha biashara zao kwa ufanisi na
kuboresha maisha ya familia zao na jamii kwa ujumla.
Katika mafunzo yaliyotolewa chini
ya mpango huu nchini kote baadhi ya wafanyabiashara wamepatiwa elimu
kuhusiana na usimamizi wa fedha binafsi unaolenga kumwezesha
mfanyabiashara kutofautisha fedha zake na biashara ili kuepusha hasara
au kufilisika, mbinu za biashara ikiwa ni pamoja na rasilimali watu na
masoko.
Vipengele vingine
walivyofundishwa ni uendeshaji wa biashara ya bia zinazoambatana na
matangazo, kumvutia mteja kwa kuweka mazingira rafiki kwa wateja na
uuzaji wa kuwajibika unaozingatia sheria za vileo, usafi na mazingira ya
afya.
Wakiongea kwa nyakati tofauti
kuhusiana na mpango huu baadhi ya wafanyabiashara waliohudhuria mafunzo
kutoka mikoa mbalimbali nchini kwa niaba ya wenzao walisema kuwa ni
mzuri na umewawezesha kupata maarifa na mbinu za kibiashara.
Samwel Tarimo mfanyabiashara wa
Mwanza akiongea kwa niaba ya wenzake waliohudhuria mafunzo hayo alisema
kuwa unasaidia kuwawezesha kujua mbinu za kuleta mafanikio katika
biashara wanayofanya na kupiga hatua ya maendeleo
“Elimu inasaidia kujua mambo
mengi na kuleta mabadiliko kwenye jamii na wafanyabiashara tuliohudhuria
mafunzo wengi wetu tumebadilika kuanzia kibiashara mpaka kimaisha kwa
kuwa kuna mambo mengi ambayo alikuwa yanatukwamisha kibiashara hasa
utunzaji wa mahesabu na kufanya mipango ya kibiashara ambayo baada ya
kuyajua mafanikio ameanza kupatikana.
Naye Jane mfanyabiashara anayeuza
vinywaji mkoani Arusha amesema mafunzo yalitotolewa kupitia mpango huu
yamewajengea uwezo wa kujiamini katika biashara wanazofanya “Huu mpango
ni mzuri na unapaswa kuigwa na makampuni mbalimbali kwa kuwa elimu
tuliyopatiwa na TBL imetufumbua macho kwa mambo mengi na wanaofuatilia
masuala waliyofundishwa hivi sasa wanakwenda vizuri kibiashara.
Monica Nyaki, mfanyabiashara wa
vinywaji mjini Moshi alisema licha ya kuwa na muda kwenye biashara yake
lakini mafunzo hayo yamempa mbinu mpya za kujenga mahusiano mazuri na
TBL, wateja na nidhamu ya pesa na usafi maeneo ya kazi na aliongeza kuwa
mafanikio katika biashara yananufaisha familia nzima ya mfanyabiashara
na jamii kwa ujumla.
Mkufunzi wa mafunzo hayo,
Nyakahinja Manyama, alisema hivi karibuni kuwa mafunzo haya
yalioendeshwa chini ya mradi wa Endelea na TBL ambao umelenga
kuwawezesha wafanyabiashara wa vinywaji kujua mbinu za biashara za
kuwawezesha kupata mafanikio ikiwemo kuwezesha kampuni kujenga uhusiano
wa karibu na wadau wakiwemo wanaosambaza vinywaji vyake.
Pia alisema mafunzo haya ni
utekelezaji wa moja ya lengo la kampuni la “kujenga dunia yenye nuru
njema lenye dhamira kuongeza kasi ya ukuaji na maendeleo kwenye jamii.
“Mradi huu wa kutoa elimu ya
biashara kwa wafanyabiashara wa vinywaji umeanza kuonesha mafanikio
makubwa kutokana na mwitikio wa wanaohitaji mafunzo haya kuwa wengi nchi
nzima na tutahakikisha tunawafikia na kuwapatia elimu hii
itakayowawezesha kupata mafanikio katika biashara zao,”alisema.
0 maoni:
Chapisha Maoni