Jumatano, 4 Mei 2016

CHUMI ASHINDA KESI YA UBUNGE JIMBO LA MAFINGA, KATIBU WA CCM AMPONGEZA

Mbunge  wa  jimbo la Mafinga mkoani Iringa Bw Cosato Chumi (kulia) akimpongeza wakili  wake Asheri Utamwa baada ya mahakama kuu kanda ya Iringa kutoa hukumu iliyompa ushindi mbunge Chumi kufuatia kesi  iliyofunguliwa na aliyekuwa mgombea  ubunge  jimbo hilo kupitia Chadema Bw Willy Mungai
Mbunge wa jimbo la Mafinga Bw Cosato Chumi akiweka sawa  bendera ya ubunge leo kabla ya kuondoka  viwanja vya mahakama kuu kanda ya Iringa baada ya  kushinda kesi ya uchaguzi ,kulia ni katibu wa CCM wilaya ya Mufindi Bw Jimson Mhagama  katibu mtoto nchini Tanzania
wakili maarufu wa Chumi Bw Asheri Utamwa (kushoto ) akizungumza na wanahabari  baada ya mteja  wake Chumi  kulia kushinda kesi ya uchaguzi  leo

Na fredy mgunda,iringa

CHAMA  cha mapinduzi  (CCM)  wilaya ya Mufindi mkoani Iringa kimempongeza mbunge wa   jimbo la Mafinga Bw Cosato Chumi baada ya kushinda  kesi  yake  ya uchaguzi  dhidi ya  aliyekuwa mgombea  ubunge jimbo  hilo  kupitia  chama  cha Demokrasia na maendeleo (Chadema) Bw Willy Mungai .

Akizungumza na wanahabari leo   nje  ya  viwanja  wa mahakama  kuu kanda ya  Iringa baada ya mahakama  kutoa  huhukumu iliyompa ushindi Bw  Chumi ,katibu  wa CCM wilaya ya  Mufindi Bw Jimson Mhagama  alisema  kuwa baada ya hukumu  hiyo ya mahakma  kumpa haki mbunge huyo  wa CCM kazi  kubwa  iliyobaki kwa  sasa ni kuona utekelezaji wa ilani ya CCM unafanywa kwa  nguvu  zote.

“Hapa  kwa  hukumu  hii haki  imeweza  kutendeka  kwani  kabla ya  kutoa  hukumu jaji alisoma na kutolea  ufafanuzi  wa  vipengele  vyote  ambavyo   mlalamikaji  alikuwa anavilalamikia  na baada ya  hapo  ndipo alipoweza  kutoa  hukumu ya kesi hiyo “

Hata  hivyo  alisema pamoja na  hukumu  hiyo  kutolewa bado wanachama wa Chadema na  wale  wa CCM katika  jimbo la Mafinga hawana budi  kuendelea  kuwa  wamoja  ili  kushikamana na mbunge  wao  kuleta maendeleo  jimboni .

Kwani  alisema suala  hilo la  kesi mahakamani   mbali ya  kuchelewesha  majukumu ya  mbunge kwa  wananchi  wake  bungeni  bado  lilikuwa  likimfanya mbunge muda  wote  kuwa ni mtu wa kuwaza  kesi  badala ya  kuwaza namna gani ya  kuwatumikia  wananchi  wake.

“ Ninawaomba   wenzetu  Chadema  wasifikilie  kukata  rufaa kuendelea na kesi   hiyo kwani katika hoja  zao  zilizopelekea  kwenda mahakamani   ufafanuzi  umetolewa  vizuri na jaji hivyo kuendelea  kukata  rufaa ni  kuendelea  kuwacheleweshea  wananchi  wa  jimbo la Mafinga  kupata maendeleo “

Pia  alimtaka  mbunge   huyo Bw  Chumi  kufidia  muda  ambao  ameupoteza kwa  kushinda mahakama  kusaka  haki kwa  kwenda  kuwatumikia  wananchi  wake kwa kasi ya hapa kazi  tu ili  jimbo  hilo lizidi  kusonga mbele kwa maendeleo.

Kwa  upande  wake Mbunge  Chumi  alisema anapenda  kuwashukuru  wananchi wake wa  jimbo la Mafinga  ambao  walitoa  ushirikiano kwa kufika mahakamani  kutoa  ushahidi  muda  wote na  kuwa zaidi anamshukuru mwenyezi  Mungu kwa  kusimamia haki katika kesi   hiyo .

0 maoni:

Chapisha Maoni