Wakala
wa Barabara nchini TANROADS Mkoa wa Dar es Salaam kupitia mpango wao w
akupunguza foleni katika jiji la Dar es Salaam, wamejidhatiti
kuakikisha wanapunguza msongano wa foleni kwa kuendelea kukarabati
barabara za pembezoni na zile za katikati kwa kiwango cha lami
ilikuondokana na foleni kwa sasa.
Akizungumza
na waandishi wa Habari Jijini Dar es Salaam leo Juni 13.2016, Mhandisi
wa miradi na madaraja wa TANROADS, Bwana Ngusa Julius amesema tayari
karibu maeneo yote ya baranara hizo taraibu zinaendelea huku maeneo
mengine zikiwa hatua ya mwisho na barabara zingine zikiwa tayari
zimekamilika na zinatumiwa kwa kiwango kikubwa kwa sasa.
Mhandisi
huyo amebainisha kuwa, foleni nyingi zinazoikumba jiji la Dar es
Salaam ni kutokana na madereva wengi kukumbia barabara za vumbi hivyo
wengi kujikuta wanatumia barabara za lami kwa kiwango kikubwa.
“Katika
jiji la Dar es Salaam barabara nyingi za mitaa ni za vumbi, na zina
mashimo makubwa ambayo yanasababisha magari kushindwa kupita. Kutokana
na hali hii madereva wa magari wanapendelea kutumia barabara za lami
zilizopo hata wanapotaka kwenda maeneo ya jirani na alipo hivyo kuwepo
na msongamano mkubwa sana kwenye barabara hizo kwa sababu kunakuwepo kwa
mwingiliano mwingi sana wa magari wakati wa kuingia na kutoka kwenye
barabara ya lami.
Ili
kupunguza msongamano wa aina hiyo, Wizara ilibuni mradi wa barabara
kupunguza msongamano katika jiji la Dar es Salaam na Wakala wa Barabara
nchini ilianza kutekeleza mradi wa ujenzi wa barabara kwa kiwango cha
lami” alieleza Mhandisi Ngusa Julius.
Aidha alizitaja barabara ambazo zimeainishwa kwenye mpango huo wa ujenzi wa barabara kuwa ni pamoja na:- Ubungo bus terminal – Kigogo – Kawawa road roundabout – (km 6.4). Kigogo Round about – Jangwani – Twiga (km 2.72), Tabata Dampo – Kigogo na Ubungo Maziwa Mabibo External (Mandela) km 2.25.
Pia zipo barabara
za Jet Corner – Vituka – Davis Corner – (km 12), Mbezi – Malambamawili –
Kinyerezi – Banana – (km 14), Old Bagamoyo na TPDC (Garden) km 9.1,
Tegeta Kibaoni – Wazo Hill – Goba – Mbezi/Morogoro Road – (km 18).
Tanki
bovu – Goba (km 9.0), Kimara Baruti – Msewe – Changanyikeni (km 2.6),
Kimara – Kilungule – External (Mabibo Mandela) km 9.0, Bunju B Mpiji
Magohe Victoria Kifulu hadi Pugu Kiltex 33.7 (Outer ringroad) na Banana –
Kinyerezi – Kifuru – (km 8)
Mhandisi
Ngusa Julius amebainisha kuwa, katika awamu za fedha baadhi ya miradi
ilianza na mingine kukamilika ikiwemo madaraja ili kusaidia kupunguza
msongamano wa magari katika jiji la Dar es Salaam.
Aidha
amebainisha kuwa, Kuchelewa kukamilika kwa mradi huu ulitokana na
wanachi wa eneo la Mchikichini kugoma kubomoa nyumba zao licha ya
kulipwa fidia kwa kufungua kesi mahakamani ya madai ya kuongezewa fidia.
“Sababu
ni nyingi ikiwemo kuchelewesha malipo ya mkandarasi kumechangia
kumaliza kazi za ujenzi mapema. Kwa sasa mkandarasi anakamilisha kazi za
ujenzi baada ya kulipwa sehemu ya madai yake zitakamilika ifikapo
mwisho mwa mwezi Juni 2016.” Alieleza Mhandisi huyo.
Kwa
upande wake Afisa Habari wa TANROADS, Bi. Aisha Malima ametoa rai kwa
wananchi kuendelea kuzitunza barabara hizo kwani zinagharimu fedha
nyingi katika ujenzi wake na pia katika utunzaji wake hivyo wananchi
wametakiwa kuchukua hatua za kuzirinda.
Maafisa
wa TANROADS wakiwa katika mkutano huo na waandishi wa Habari leo Jijini
Dar es Salaam kuelezea namna ya kupunguza msongamano wa foleni
Mhandisi
wa miradi na madaraja wa TANROADS, Bwana Ngusa Julius akielezea namna
walivyoweza kujenga barabara kwa kiwango cha lami katika jiji la Dar es
Salaam sambamba na madaraja yanayounganisha barabara hizo.
Mhandisi
wa miradi na madaraja wa TANROADS, Bwana Ngusa Julius (kushoto)
akifafanua jambo, kulia kwake ni Afisa Habari wa TANROADS, Bi. Aisha
Malima. (Picha zote na Andrew Chale]
0 maoni:
Chapisha Maoni