Jumatano, 1 Juni 2016

Hifadhi ya Selous yapoteza asilimia 90 ya Tembo wake


imagesNa Daudi Manongi
Hifadhi ya Taifa ya  wanyamapori ya Selous iliyopo kusini mwa Tanzania imepoteza asilimia  90 ya Tembo waliopo katika hifadhi hiyo kutokana na ujangili uliokithiri.
Ripoti ya mfuko wa hifadhi ya wanyapori na mazingira duniani (WWF) imesema kufikia mwaka 2022 kama hakutakuwa na hatua zozote kali zitakazochukuliwa kuwalinda tembo kutokana na ujangili  basi  watatoweka kabisa.
Ripoti hiyo imeendelea kusema kuwa kwa miaka ya nyuma mbuga ya Selous ilikuwa mojawapo ya mbuga kubwa kabisa katika bara la afrika yenye tembo wengi ambapo kulikuwa na tembo zaidi ya 110000 lakini kutokana na ujangili uliokithiri katika miaka 40 iliyopita tembo hao wamepungua na kubakia 15000 tu uku mahitaji makubwa ya pembe za ndovu katika nchi ya china yakitajwa na ripoti hiyo kuwa kichocheo kikubwa cha ujangili na mauaji ya idadi kubwa ya tembo hao.
Aidha ripoti hiyo inaonyesha hathari kubwa  kiuchumi itakayotokea  kutokana na kwamba Tanzania kupitia Mbuga ya Selous inaingiza dola milioni 6 kwa mwaka ikilinganishwa na Sekta ya Viwanda inayochangia dola bilioni 5 katika pato la Taifa.
Pamoja na Hayo Serikali ya awamu ya tano  kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii imeweka mikakati madhubuti ikiwemo kuunda kitengo chake cha intelijensia na kuunda kanda nane za doria za ushirikiano katika mifumo ya ikolojia ya mbuga ya Selous ambayo imeanza kuwa na mafanikio  ikiwa ni pamoja na kushirikiana na wadau wa uhifadhi kuwezesha upatikanaji wa vitendea kazi na zana kwa ajili ya doria.
Mwaka 2014 Shirika la Kimataifa la Sayansi,Elimu na Utamaduni la umoja wa mataifa(UNESCO) liliiweka Mbuga ya Selous katika Urithi wa asili ulio hatarini Duniani.

0 maoni:

Chapisha Maoni