Alhamisi, 23 Juni 2016

HARAMBEE YA OKOA MAISHA YA WAANDISHI WA HABARI KUFANYIKA JUMAMOSI JUNI 25 MKOANI DODOMA


Mjumbe wa kamati ya maandalizi ya kampeni ya Okoa Maisha ya waandishi wa habari,Peter Nyanje akizungumza mbele ya Waandishi wa habari (hawapo pichani) leo jijini Dar kuhusiana na maandalizi ya harambee maalumu ya kuosha magari yaani Media Car wash for health, litakalofanyika Mjini Dodoma, Uwanja wa Jamhuri, siku nzima ya Jumamosi June 25, 2016. Pichani shoto ni Mratibu wa Kampeni hiyo Grace Nackson na kulia ni Mratibu kutok Kampuni ya Midia Assistant,Dickson Matikila pamoja na Msanii wa muziki wa kizazi kipya atambulika kwa jina la kisanii Inspekta Haroun.PICHA NA MICHUZI JR.
Mratibu wa Kampeni ya Okoa Maisha ya waandishi wa habari, Grace Nackson akitoa ufafanuzi zaidi kuhusiana na harambee hiyo kwa waandishi wa Habari waliotaka kufahamu zaidi kuhusiana na harambee hiyo inayotarajiwa kufanyika Mjini Dodoma, Uwanja wa Jamhuri, siku nzima ya Jumamosi June 25, 2016.Mratibu huyo ameeleza kuwa Lengo la harambee hiyo ni kukusanya fedha zitakazotumika kuwakatia Bima ya Afya waandishi wa habari takribani 1000 hapa nchini.
Msanii wa muziki wa kizazi kipya atambulikae kwa jina la kisanii Inspekta Haroun akifafanua jambo kuhusiana na ushiriki wao kama sehemu ya wasanii watakaoshiriki siku hiyo mjini Dodoma.
Mkutano ukiendelea kuhusiana na harambe hiyo.
 
======  ======  ======  ======
Kamati ya Maandalizi ya Okoa Maisha ya waandishi wa habari, imeandaa harambee maalumu ya kuosha magari yaani Media Car wash for health, litakalofanyika Mjini Dodoma, Uwanja wa Jamhuri, siku nzima ya Jumamosi June 25, 2016. 
 
Lengo la harambee hiyo ni kukusanya fedha zitakazotumika kuwakatia Bima ya Afya waandishi wa habari takribani 1000 hapa nchini. Kamati ya Maandalizi ya harambee inajumuisha waandishi wa habari kutoka vyombo mbali mbali vya habari chini ya Uenyekiti wa Bw. Benjamin Thompson Kasenyenda, inaomba ushirikiano wakaazi wa Dodoma pamoja na Wabunge. Mtakumbuka kwamba kamati hii ilifanya tukio kama hili viwanja vya Leaders, Jijini Dar es Salaam July 4, 2015, ambapo zaidi ya 30m/-, zilichangishwa.
 
Fedha hizo zilisaidia gharama za matibabu ya waandishi watatu waliokuwa mahututi wakati huo, mmoja wao akiumwa kansa. Lengo la mwaka huu limebadilika ambapo tumekusudia kuhakikisha kuwa wengi wao wanakatiwa bima ya afya, ili kujikinga na kadhia ya kuchangiwa fedha pale wanapofikwa na maradhi. Aidha, kwenye changizo hili tutakuwa na kadi maamlum za kuomba michango ya mfuko huo, ambazo tutazigawa kwa Wabunge kupitia ofisi ya Bunge. Tutaomba ushirikiano mzuri kutoka kwa Wabunge na wakazi wa Mji wa Dodoma ili kufanikisha zoezi hili. 
 
Pia tumeandika barua kwa Spika tukimwomba awajulishe Wabunge ili wajitokeze kwa wingi kwenye zoezi hili. Waratibu wa Harambee ile ambayo ni Kampuni ya Media Assistant, imefanya utaratibu wa kumleta Miss Tanzania Ms Lilian Kamazima pamoja na wasanii wa Bongo Movies na Bongo Fleva kuja kushiriki zoezi hilo. 
 
Wasanii hao ni kundi la Weusi ambalo linajumuisha John Simon Makini a.k.a Joh Makini, Nickson Simon a.k.a Nikki wa Pili na George Sixtus Mdemu a.k.a G Nako, wenye asili ya Arusha na wanafanya shughuli zao za kimuziki Jijini Dar es Salaam pamoja na Haruna Kahena a.k.a Inspekta Haruni. Wasanii wa Bongo Movies ni pamoja na Aunt Ezekiel, Kajala Masanja, Ray Kigosi na Jacob Stephen a.k.a JB. Na pia kutoka Orijino Komedi tumepewa mwakilishi Isaya Mwakilasa ambaye zaidi anajulikana kwa jina la Wakuvanga na maarufu zaidi kama Mama Bele. Asanteni kwa Kunisikiliza Judicate Shoo, Mjumbe wa Kamati ya Maandalizi ya Harambee

0 maoni:

Chapisha Maoni