Waziri
wa Afya Zanzibar Mahmoud Thabit Kombo akizungumza na wafanyakazi katika
hafla ya kuamuaga Katibu Mkuu aliemaliza muda wake Dkt. Mohd Jidawi
(kushoto) na kumkaribisha Katibu Mkuu mpya (kulia) Dkt. Juma Malik Akili
alievaa kofia katika Ofisi ya Wizara hiyo Mnazimmoja, Mjini Zanzibar.
Katibu
Mkuu Mstaafu wa Wizara ya Afya Dkt. Mohd Jidawi akiwashukuru
wafanyakazi wa Wizara hiyo kwa ushirikiano mkubwa waliompa wakati wa
kutekeleza majukumu yake.
Waziri
wa Afya Mahmoud Thabit Kombo na Katibu Mkuu mpya wa Wizara hiyo Dkt.
Juma Malik Akili wakimsikiliza katibu Mkuu mstaafu Dkt. Mohd Jidawi
(hayupo pichani) wakati wa hafla ya kumuaga iliyofanyika Wizara ya Afya
Mnazimmoja.
Waziri
wa Afya Mahmoud Thabit Kombo akimkabidhi cheti cha heshima Katibu Mkuu
mstaafu wa Wizara hiyo Dkt. Mohd Jidawi katika hafla ya kumuaga
iliyofanyika Wizarani, Mnazimmoja. Wa kwanza (kushoto) ni mke wa Dkt.
Jidawi, Dkt. Mwanaheri Jidawi.
0 maoni:
Chapisha Maoni