Mwalimu wa shule ya Msingi Ikula akiwa na mbunge Mwamoto
Na MatukiodaimaBlog
MBUNGE wa Kilolo mkoani
Iringa amechangia kiasi cha Tsh
milioni 1 kwa ajili ya ukarabati
wa shule ya
Msingi Mazombe ambayo viongozi
mbali mbali wamesoma katika shule
hiyo akiwemo aliyekuwa mbunge
wa jimbo hilo kabla yake Prof Peter
Msolla huku kiasi cha Tsh milioni milioni 7 zikitolewa kwa shule ya Kiheka sekondari
na shule ya msingi Ikuvala kwenye kata ya Nyalumbu inayoongozwa na diwani wa chama cha
Demokrasia na maendeleo (chadema)
Mwamoto ambaye katika ziara
yake ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo inayoendelea
katika jimbo hilo la
Kilolo ametumia kiasi cha Tsh milioni 45 za
mfuko wa jimbo
kuunga mkono jitihada mbali mbali za
wananchi wake alisema kuwa huu si
wakati wa siasa ni wakati wa kuwatumikia wananchi wote bila
kuwabagua kwa itikadi za kisiasa
.
Akizungumza na
uongozi wa shule ya Msingi Mazombe jana
baada ya kufanya ziara ya ghafla
shuleni hapo kukagua shule
hiyo alisema haitapendeza kuona
anaitelekeza shule hiyo ambayo ni
shule aliyosoma mtangulizi wake
katika ubunge Prof Msolla hivyo kuahidi kuikarabati vizuri na
kuwa shule yenye ubora
kama shule nyingine .
“Natambua
mchango wa Prof Msolla katika wilaya ya Kilolo na Taifa itakuwa
si busara kwangu kama mbunge kushindwa
kuikarabati shule hii ya Mazombe …..naomba ukarabati
uanze mara moja kwa
kuweka madirisha na
sakafu nzuri nje ya hii ambayo ni mashimo mashimo” alisema mbunge
huyo
Kuwa kwa ajili ya kuonyesha kuwa huu ni
wakati wa kazi kwa kila
kiongozi kuwatumikia wananchi
bila kuwabagua kwa itikadi zao amefika katika ya Nyalumbu
ambayo ni moja kati ya kata
mbili za wilaya ya Kilolo zinazoongozwa na madiwani wa
Chadema na kuchangia
miradi ya maendeleo inayoendelea katika kata hiyo .
Hivyo aliwataka wananchi
na wanasiasa katika
wilaya ya Kilolo kwa sasa
kuungana pamoja kuleta maendeleo kwani
huu si wakati wa siasa ni wakati
wa wanasiasa kuwatumikia wananchi wao kwa
vitendo si maneno .
Katika shule ya
msingi Ikula mbunge huyo amechangia Tsh milioni 1 ili
kukamilisha ujenzi wa
vyoo vya wanafunzi shuleni hapo
huku akieleza kusikitishwa na mvutano wa madaraka
katika kijiji hicho
na kupelekea wananchi kushindwa
kuendelea na ujenzi wa nyumba ya
mwalimu kwa zaidi ya miaka miwili
sasa nyumba kutokamilika .
Hivyo alisema
atamjulisha mkuu wa wilaya na
mkurugenzi ili kufika kutatua mgogoro huo na
kuona namna gani Halmashauri
inaweza kuunga mkono jitihada za
wananchi hao hasa kumalizia
nyumba hiyo na wodi ya wazazi japo
kwa upande wake
ameahidi kutoa bati za kuezekea nyumba hiyo ya
mwalimu itakapomalizika.
Mwakilishi wa mkurugenzi
mtendaji wa Halmashauri ya Kilolo Henry Kaywanga alisema kuwa Halmashauri
ya Kilolo imechangia miradi mbali mbali ya maendeleo ya wananchi
kiasi cha Tsh milioni 120 zilizotumwa kama ruzuku ya
serikali (LGDG-CDG) .
Alisema baadhi ya
maeneo miradi imekuwa ikisuasua
kutokana na migogoro ya viongozi na kuwa
jitihada za kufika katika
maeneo hayo yenye migogoro
zimekuwa zikifanyika na
katika kijiji cha Ikula watafika kushughulikia mgogoro huo.
Mkuu wa wilaya ya
Kilolo Asia Abdalah akizungumza
na mwandishi wa habari
hizi kwa njia ya simu
juu ya ombi la wananchi wa Ikula
kutaka kufika kumaliza tofauti zao alisema
kuwa toka ameteuliwa kuwa
mkuu wa wilaya ya Kilolo na mheshimiwa Rais Dkt John Magufuli amekuwa hakai ofisini
kila siku ni kuzungukia wananchi vijijini na kuwa
kijiji hicho ni miongoni mwa vijiji ambavyo vipo kwenye ratiba
wakati wowote kuanzia sasa atafika .
Alisema kuwa kuna baadhi ya maeneo alifika na kutoa maagizo ya kukamilisha
miradi na tayari miradi husika
imekamilishwa na kutolea mfano
kijiji cha Mahenge wanafunzi wa
awali shule ya msingi Mlowa walikuwa
wakisomea chini ya mti na katika ziara yake alitoa agizo la kujenga vyumba viwili
vya madarasa ndani ya mwezi mmoja na wananchi wamekamilisha ujenzi huo ndani ya wiki tatu pekee.
|
0 maoni:
Chapisha Maoni