WAKATI
Bunge la Tanzania wiki hii linatarajiwa kujadili na kupitisha muswada
wa habari, Shirika la Umoja wa mataifa la Elimu, sayansi na Utamaduni
(UNESCO) limehadharisha juu ya uwapo wa sheria zinazotishia uhuru wa
vyombo vya habari.
Akizungumza
katika kongamano linalohusu ukatili kwa waandishi ikiwa ni maadhimisho
ya siku ya kupinga ukatili kimataifa kwa waandishi wa habari, Mkuu wa
idara ya mawasiliano na habari wa UNESCO, Ofisi za Tanzania, Christophe
Legay alisema katika utekelezaji wa maendeleo endelevu sekta ya habari
ni muhimu na hivyo watendaji wake wanatakiwa kuwekewa mazingira huru ya
kiutendaji.
Serikali
ya Tanzania imepeleka muswada wa habari ambao unalalamikiwa na wadau wa
habari kwamba haukupatiwa muda wa kutosha wa kujadiliwa na kuondolewa
kwa vipengele ambavyo vinawanyima waandishi wa habari uwezo wa kuandika.
Mkuu
wa idara ya mawasiliano na habari wa UNESCO, Ofisi za Tanzania,
Christophe Legay akizungumza machache kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi
kufungua kongamano linalohusu ukatili kwa waandishi ikiwa ni maadhimisho
ya siku ya kupinga ukatili kimataifa kwa waandishi wa habari,
lililofanyika jana jijini Dar es Salaam.
Aidha
ndani ya muswada huo imeelezwa na Jukwaa la Wahariri kwamba kuna
vipengele ambavyo vinakwamisha umahiri wa uandishi na uchunguzi kama
kufutiwa kwa leseni na kuuzwa kwa mitambo kutokana na makosa mbalimbali
ambayo yamegeuzwa ya jinai.
Aidha
wadau hao wanasema kwamba serikali imejitengenezea nafasi ya kuwa na
nguvu kubwa ya kudhibiti habari kupitia Kurugenzi ya Maelezo na Waziri
mwenyewe huku Bodi iliyopangwa kuwa huru ikionekana kwamba haina nguvu
zakutosha.
Akizungumza
haja ya mazingira rafiki Legay alisisitiza kuwaTaifa linastahili
kuhakikisha kwamba kumewekwa mazingira rafiki ya upatikanaji wa habari
na kwamba kila mwananchi anapata haki yake ya kupata, kusambaza habari
kwa mujibu wa mikataba ya kimataifa na sheria zinazohusu habari za
taifa.
Kaimu
Mkurugenzi Idara ya Habari Maelezo, Jamal Zuberi akizungumza akifungua
kongamano linalohusu ukatili kwa waandishi ikiwa ni maadhimisho ya siku
ya kupinga ukatili kimataifa kwa waandishi wa habari kwa niaba ya Katibu
Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Prof. Elisante Ole
Gabriel, lililofanyika jana jijini Dar es Salaam.
Alisema
ingawa haki ya kupata habari imeelezwa waziwazi katika Katiba ya
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia vifungu 18 na 21 mambo
yanayojitokeza sasa katika sheria za habari nchini Tanzania yanatishia
haki hiyo, kutokana na sheria hizo kuonekana kubana uchakataji wa
habari. Akitolea mfano wa sheria ya huduma ya habari ya mwaka 2016.
Alisema
katika mkakati wa utekelezaji wa malengo endelevu ya dunia kuna mpango
mkakati wa kulinda waandishi wa habari na upatikanaji wa habari kama
ilivyoelezwa katika lengo namba 16, kifungu kidogo cha 10.
Alisema
kwa sasa dunia inakabiliwa na tishio kubwa la upatikanaji wa habari
kutokana na vitisho vinavyowekwa kwa waandishi wa habari ikiwa na pamoja
na kuuawa, kutiwa kizuini au kupotea bila kujulikana.
Alisema
katika muongo mmoja uliopita waandishi 827 waliuawa na kwamba ni
asilimia 7 tu ya mauaji hayo yalipatiwa ufumbuzi. Aidha alisema mwaka
jana ulikuwa mwaka mbaya zaidi kwa waandishi wa habari, huku waandishi
16 pekee wakiuawa katika bara la Afrika.
Mkurugenzi
wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu (THRDC), Onesmo Olengurumwa
akijadili rasimu ya mkakati wa mpango wa usalama wa waandishi wa habari
wakati wa kongamano linalohusu ukatili kwa waandishi ikiwa ni
maadhimisho ya siku ya kupinga ukatili kimataifa, lililofanyika jana
jijini Dar es Salaam.
Alisema
kitendo cha kuwadhibiti waandishi wa habari kunaashiria udhibiti wa
upatikanaji wa habari huru ambao ndio msingi wa demokrasia na maendeleo
ya jamii.
Aliitaka
jamii kuhakikisha kwamba inakaa pamoja na kuona haja ya kulinda uhuru
wa habari ikiwa na pamoja na kuwalinda wachakataji habari ili kila mtu
anayetaka kupata habari aweze kuipata na kuitumia kwa maendeleo yake,
jamii na taifa.
Akimkariri
Mkurugenzi Mkuu wa Unesco Irina Bokova, mkuu huyo wa mawasiliano
alisema kwamba ukatili na vitendo vinavyoshabihiana navyo dhidi ya
waandishi wa habari ni kinyume na uhuru na haki ya upatikanaji wa
habari na wanaofanya mambo hayo wanatishia utawala bora wa kisheria na
kusababisha utoaji habari usiokamili kwa hofu ya udhibiti na matokeo
yake jamii nzima inapotoka na kuhangaika. Leo hii tunahitaji dhamira
mpya ya kuhakikisha kwamba tunatengeneza mazingira salama na rafiki kwa
waandishi wa habari.
UNESCO
ni mdau mkubwa wa habari nchini Tanzania na katika taarifa yake kwa
vyombo vya habari ilikumbushia kazi inayofanya pamoja na wadau wengine
wa habari wakiongozwa na Tanzania Human Rights Defenders Coalition
kutengeneza mpango kazi wa ushawishi wa namna bora ya kuchakata na
kufanyakazi ya uandishi wa habari nchini Tanzania.
Mdau
wa tasnia ya habari, Kenneth Simbaya akiwasilisha fursa na changamoto
walizokumbana nazo wakati wa uandaaji wa rasimu ya mkakati wa mpango wa
usalama wa waandishi wa habari katika kongamano linalohusu ukatili kwa
waandishi ikiwa ni maadhimisho ya siku ya kupinga ukatili kimataifa,
lililofanyika jana jijini Dar es Salaam.
Kutokana
na mkakati huo mwaka jana kuliundwa kikosi kazi cha kuangalia usalama
wa waandishi wa habari na taarifa inatarajiwa kutolewa wakati wowote
kuanzia sasa namna bora ya kuwawezesha waandishi wa habari kufanyakazi
kwa usalama.
Naye
msemaji wa serikali ya Tanzania akizungumza Kaimu Mkurugenzi Idara ya
Habari Maelezo, Jamal Zuberi akizungumza kwa niaba ya Katibu Mkuu Wizara
ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Prof. Elisante Ole Gabriel
katika tukio hilo alitoa wito kwa taasisi zisizo za kiserikali, taasisi
za sheria na vyombo vya habari kuhakikisha kwamba mazingira ya kufanyia
kazi waandishi wa habari ni salama na haki za upatikanaji wa habari
haudhibitiwi.
Alisema
ili kuwezesha hali hiyo serikali imepeleka muswada wa waandishi wa
habari bungeni na pia ikiwa kama moja ya nchi iliotia saini mikataba ya
kimataifa kuhusu upatikanaji wa habari serikali itafanyakazi kwa pamoja
na wadau kuhakikisha kwamba waandishi wa habari wanapata mazingira
rafiki na salama ya kufanyia kazi.
Mmoja
wadau wa masuala ya sheria akizungumza jambo katika kongamano
linalohusu ukatili kwa waandishi ikiwa ni maadhimisho ya siku ya kupinga
ukatili kimataifa kwa waandishi wa habari, lililofanyika jana jijini
Dar es Salaam.
Mwanasheria
kutoka Nola, James Marenga akifafanua jambo wakati wa kongamano
linalohusu ukatili kwa waandishi ikiwa ni maadhimisho ya siku ya kupinga
ukatili kimataifa kwa waandishi wa habari, lililofanyika jana jijini
Dar es Salaam.
Kaimu
Mkurugenzi Idara ya Habari Maelezo, Jamal Zuberi (kushoto) akiwa na
wadau wa tasnia ya habari wakati wa kongamano linalohusu ukatili kwa
waandishi ikiwa ni maadhimisho ya siku ya kupinga ukatili kimataifa kwa
waandishi wa habari, lililofanyika jana jijini Dar es Salaam.
Wadau
wa tasnia ya habari na masuala ya Sheria walioshiriki kwenye kongamano
linalohusu ukatili kwa waandishi ikiwa ni maadhimisho ya siku ya kupinga
ukatili kimataifa kwa waandishi wa habari, lililofanyika jana jijini
Dar es Salaam.
Washiriki
wakitazama moja ya video ya shuhuda inayozungumzia usalama wa waandishi
wa habari wakati wa uchaguzi wakati wa kongamano linalohusu ukatili kwa
waandishi ikiwa ni maadhimisho ya siku ya kupinga ukatili kimataifa,
lililofanyika jana jijini Dar es Salaam.
0 maoni:
Chapisha Maoni