HUDUMA
ya upandikizwaji wa vifaa vya usikivu kwa watoto imeanza kutolewa rasmi
nchini katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili baada ya wataalamu wa
huduma hiyo kurejea wakitokea mafunzoni nchini India ili kuweza kusaidia
watanznia hususani watoto wenye matatizo ya kusikia.
Akizindua
huduma hiyo kwenye hafla fupi iliyofanyika jijini Dar es salaam Katibu
Mkuu wa Wizara ya Afya , Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Dkt.
Mpoki Uisubisya amesema kuwa Huduma hiyo imekua hadimu nchini hivyo
kufanya kugharamia kiasi kikubwa cha fedha kwenda kuwatibia nje ya nchi.
“Kwakweli
huduma hii ya kupandikiza watoto vifaa vya usikivu italeta msaada
mkubwa kwa watanzania na kuokoa gharama takribani shilingi milioni 80
kwa kila mtoto ambaye alitakiwa kwenda kutibiwa nje ya nchi” alisema
Dkt. Ulisubisya.
Aidha
Dkt. Ullisubsya amesema kuwa wazazi wanatakiwa kuwa mstari wa mbele
kugundua mapema matatizo ya watoto na kuwaleta katika Hospitali ya
Muhimbili ili wapate taratibu za kupata huduma hiyo bila ya kuchelewa na
kpata madhara makubwa.
Kwa
upande wa Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Muhimbili Prof. Lawrence
Museru amesema kuwa Huduma hiyo ambayo ilikua inafuatwa nje ya nchi sasa
inafanyika nchini ikiwa ni jitihada za serikali katika kuokoa gharma za
matibabu ya nje ya nchi.
Aidha
Prof. Museru amesema kuwa hadi kufikia Januari 2017 MNH itaanza kufanya
upasuaji na kupandikiza vifaa vya usikivu ikiwa ni huduma iliyokamilika
bila ya kwenda nje ya nchi hivyo kupelekea kupunguza gharama zaidi na
kusogeza huduma karibu.
“Hapa
tulipofikia sio mwisho wa kutoa hudum hii , tunataka kufikia Januari
2017 tuwe tunafanya upasuaji kabla ya kupandikiza vifaa vya usikivu
ikiwa ni huduma kamili na tutakuwa tumefikia baadhi ya malengo
tuliyojiweka mpaka kufikia muda huo” alisema Prof. Museru
Aidha
Prof. Museru amesema kuwa Serikali ilianza jitihada za kuileta huduma
hii nchini miaka mitatu iliyopita kwa kushirikiana na kampuni ya kuuza
vifaa vya kupandikiza vifaa vya usikivu ya Medel kutoka nchini Misri.
Kwa
upande wa Mzazi wa mtoto aliyepandikizwa kifaa cha usikivu Angel
Ibrahimu (4) mkazi wa Mbeya amesema kuwa anaishukuru Serikali kwa
jitihada zake za kufanikisha huduma hiyo kwa mtoto wake kwani lilikua
tatizo ambalo hakuweeza kulitatua kwa uwezo wake.
Katika
ufunguzi wa huduma hiyo ambayo itakua endelevu nchini imepandikiza
vifaa vya usikivu kwa watoto 16 ambao wapepunguza gharama ya kwenda nje
ya nchi takribani shilingi milioni 300 ambazo zitaenda kwenye huduma
nyingine za maendeleo ya jamii.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia , Wazee na Watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya akiongea na waandishi wa habari hawapo pichani wakati wa uzinduzi wa huduma ya upandikizwaji wa vifaa vya usikivu kwa watoto uliofanyika jijini Dar es salaam, kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Muhimbili Prof. Lawrence Museru.
Mkurugenzi wa kampuni inayotoa huduma na kuuza vifaa vya usikivu ya Medel Bw. Mohamed Disouky wa kwanza kushoto akimpa maelezo Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia , Wazee na Watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya wa pili kulia jinsi huduma hiyo inavyotolewa wakati wa uzinduzi wa huduma ya upandikizwaji wa vifaa vya usikivu kwa watoto uliofanyika jijini Dar es salaam, wa kwanza kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Muhimbili Prof. Lawrence Museru.
Baadhi ya wazazi wa watoto wenye matatizo ya usikivu wakiwa katika foleni ya kusubiri huduma ya upandikizwaji wa vifaa vya usikivu wakati wa uzinduzi wa huduma ya upandikizwaji wa vifaa vya usikivu kwa watoto uliofanyika jijini Dar es salaam.
Picha zote Na Ally Daud-MAELEZO
0 maoni:
Chapisha Maoni