Posted by Esta Malibiche on Nov 4,2016 in NEWS
Pendo Kilezu Muuguzi na mtoa huduma kwa walemavu wa ngozi katika Hospital ya Rufaa mkoa wa Iringa,akitoa Elimu jinsi ya matumizi ya mafuta ya ngozi kwa walemavu wa ngozi Albino,aliwataka na kusema kuwa, kumekuwa na wimbi kubwa la baadhi ya
wazazi kuwaficha watoto ndani wenye ulemavu wa ngozi Albino,na hatimae kushindwa
kuwapatia matibabu na mahitaji muhimu yanayostahili kama binadamu wengine.
Pendo Kilezu Muuguzi na mtoa huduma kwa walemavu wa
ngozi katika Hospital ya Rufaa mkoa wa Iringa,akiendelea na zoezi la kutoa Elimu juu ya kupaka mafuta.
Picha zote na Esta Malibiche [KALI YA HABARI BLOG]
Na Esta Malibiche
Iringa
Wazazi wametakiwa kutowaficha watoto wenye ulemavu wa ngozi
Albino,bali wawapeleke katika vituo vya Afya ili waweze kupata matibabu pamoja na vifaa vyakujikinga na jua ili wasiweze kuathirika na mionzi ya jua.
Hayo yamesemwa jana na Daktari wa magonjwa ya Ngozi na via vya
Uzazi Dkt.Pili Shing’oma wakati wa akitoa Elimu kwa wazazi na watu wenye ulemavu wa ngozi juu ya kujikinga na Saratani ya Uzazi
na Clinic ya watu wenye ulemavu wa Ngozi uliofanyika jana katika Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa
Iringa.
Sheng’oma alisema kuwa kumekuwa na wimbi kubwa la baadhi ya
wazazi kuwafika watoto ndani yenye ulemavu wa ngozi Albino,na kushindwa
kuwapatia matibabu na mahitaji muhimu yanayostahili kama binadamu wengine.
Alisema kumekuwa na vitendo vya kikatili na unyanyasaji
usiostahili dhidi yao walemavu wa ngozi kuuawa na wengine kutengwa na familia
zao kutokana na ulemavu huku baadhi ya wananchi wakishiriki mambo ya
kishirikina kuwakata baadhi ya viongo.
Alisema wanakabiliwa na changamoto ya ukosefu wa usafiri na
nauli ili kuwafikia walemavu waliopo vijijini na kuwapatika huduma ya matibabu
pamoja na vifaa mbalimbali.Hivyo aliwaomba wadau kujitokeza kusaidia ili Elimu
juu ya kujikinga na mionzi ya jua kwa walemavu wa ngozi itolewe hadi vijijini
ili kuiokoa jamii.
‘’’’’Tunashindwa kuwafikia wote kila wilaya na vijiji
kutokana na kutokuwa na bajeti ya usafiri na nauli.Naiomba Serikali iguswe
katika hili,pia ninawaomba wazazi kuwaleta watoto wao katika clinic na waache kuwaficha ndani kwani mlemavu wa
ngozi anatakiwa kupata huduma hii’’’’’Alisema Shing’oma
Kwa upande wake katibu wa chama cha watu wenye ulemavu wa
Ngozi [TAS]Mkoa wa Iringa Leonansi Sambala alilishukuru shirika la USAID kwa
kuwapatia vifaa vinavyosaidia watu wenye ulemavu wa ngozi kujikinga na mionzi
ya jua ambayo inaweza letya athari kubwa kwao wakati wakifanya shughuli za
maendeleo pamoja na wanafunzi.
‘’’’Mradi huu kutoka shirika la USAID ulipoanza ulilenga
kumfikia kila mlemavu wa ngozi,pamoja na wafadhirikuleta mafuta tumeshindwa
kuwafikia watu wenye ulemavu wa ngozi vijijini,hivyo tunaiomba serikali
itusaidie na wadau watusaidie kusafirisha Albino walioko vijijini kuwaleta katika
Hospitali ili waweze kupata huduma’’’’’’Alisema Sambala
Sambala aliwasihi Walimu kuwasaidia wananfunzi ambao ni
walemavu wa ngozi kutowapa adhabu ya kukaa juani kwa muda mrefu,pia kuwapa
kipaumbele kukaa mbele ya darasa kutokana na uono hafifu walionao ili waweze
kusoma na kusikiliza kile kinachofundishwa.
‘’’’’Kwa mkoa wa Iringa walemavu wa Ngozi wapo 378 huduma
haziwafii wote kutokana na swala la uwezashwaji kuwa ngumu,ikiwa nipamoja na
baadhi ya wazazi kushindwa kuwaleta watoto wao katika Hospitali kwa ajili ya
clinic’’’’’’alisema Sambala
0 maoni:
Chapisha Maoni