Posted by Esta Malibiche on Nov4,2016 in NEWS
Na Eleuteri Mangi- MAELEZO
Muwada wa Sheria ya Huduma za
Habari wa mwaka 2016 umesomwa mara ya pili Bungeni mjini Dodoma ukiwa na
lengo la kuifanya tasnia ya habari nchini kuwa taaluma kamili.
Wiziri wa Habari, Utamaduni,
Sanaa na Michezo Nape Nnauye amesema hay oleo Bungeni Dodoma alipokuwa
akiwasilisha Muswada huo, huku akisisitiza kuwa una sehemu kuu nane
ambazo zinaufanya kuleta mageuzi katika tasnia ya habari nchini na
kuifanya kuwa taaluma kamili itayowaletea heshima wanahabari na tasnia
hiyo kwa ujumla.
“Hatuwezi kwa na vyombo vya habari makini kama hatutakuwa na wanahabari wenye taaluma ya habari nchini” alisema Nape.
Katika kuonesha ushirikishwaji wa
wadau katika kutoa maoni yaliyolenga kuboresha Muswada huo, Waziri Nape
amesema kuwa kumekuwa na ushirikishwaji mkubwa wenye wigo mpana kutoka
kwa mwananchi mmoja mmoja, wanataaluma wa habari, wanasheria kupitia
Chama cha Mawakili Tanzania (TLS), Baraza la Habari Tanzania (MCT),
Umoja wa Wamiliki wa vyombo vya habari (MOAT) na Taasisi ya Wanahabari
Kusini mwa Afrika, tawi la Tanzania (MISA-TAN).
Wadau wengine walitoa maoni yao
ni Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Sikika, Wabunge kupitia
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii pamoja na
michango ya Wabunge kupitia Kamati nyingine ambao umesaidia katika
kuboresha Muswada huo wenye dhamira ya kuleta ufanisi katika sekta ya
habari.
Miongoni mwa maeneo ambayo wadau
hao wameyafanyia maboresho ili Muswada uwe na tija ni pamoja na
kuainisha haki na wajibu wa wananhabari ikiwemo uhuru wa kukusanya,
kuhariri na kuchapisha au kutangaza habari pamoja na kuainisha haki ya
chombo cha habari kukata rufaa kwa kuzingatia mfumo wa wazi na wa
kidemokrasia kupitia vyombo vya kutoa haki ikiwemo mahakama huku Jaji
Mkuu akiweka utaratibu wa kusikilizwa haraka kwa kesi za masuala ya
kihabari.
Maboresho mengine yaliyofanya ni
uwakilishi wa wanahabari katika Bodi ya Ithibati kwa kuzingatia uwiano
wa wajumbe kutoka sekta ya habari ya umma na ya binafsi, kuviondolea
adhabu vyombo vya habari au wamiliki baadhi ya makosa ya mwandishi
ambapo atawajibishwa na Bodi ya Ithibati akiwa yeye ni mwanataaluma
kamili kukutenda makosa ya kimaadili na vyombo vya dola kukamata mitambo
na vifaa vya wanahabari maboresho yanaonesha kazi hiyo sasa itafanywa
na Jeshi la Polisi kwa sheria ya Mwenendo wa Mkosa ya Jinai badala ya
kazi hiyo kufanywa na Mkurugenzi wa Idara ya Habari.
Zaidi ya maboresho hayo, Waziri
Nape ameongeza kuwa maboresho mengine ni kuhusu mitambo kutohusika moja
kwa moja kwa kosa la gazeti ambalo limechapisha habari yenye makosa ya
kisheria dhidi ya watu au taasisi mbalimbali.
Waziri Nape amefafanua kuwa
chimbuko, muktadha na mchakato wa kuandaa Muswada huo unatokana na
baadhi ya vipengele vya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania baada
ya kufanyiwa marekebisho mwaka 1984 ambapo haki ya kikatiba ya kutafuta,
kupokea na kutoa habari imeainishwa kwenye Ibara ya 18 (b) pamoja na
mikataba mbalimbali ya kimataifa ya inayoainisha haki na wajibu wa sekta
ya habari.
Mkatabahiyo ya Kimataifa ni ule
wa Haki za Kisiasa na Kiraia wa mwaka 1966 ambao Tanzania iliuridhia
Juni 11, 1984 pamoja na Mkataba wa Afrika wa Haki za Binadamu na Watu
1981 ambao nao uliridhiwa Februari 18, 1984.
Akinukuu maneno mbalimbali ya
watu maarufu duniani juu ya masuala ya habari akiwemo Rais wa Marekani
Thomas Jefferson Januari 16, 1789, Rais wa zamani wa Afrika Kusini
Nelson Mandela, Muasisi wa Taifa la India Mahatma Ghandhi, Baba wa Uhuru
wa Habari John Stuart Mill (1806-1873) pamoja na Baba wa Taifa Mwalimu
Julius Nyerere, Waziri Nape akinukuu maneno ya mmoja wa viongozi hao
Mahatma Ghandhi aliamini kuwa uhuru wa kweli wa kujieleza ni ule
unaoweka mbele heshima ya watu wengine na kuwalinda dhidi ya dhara,
kebehi, kejeli na madhara mengine huku Baba wa Uhuru wa Habari John
Stuart Mill akibainisha dhima ya uhuru wa vyombo vya habari na umuhimu
wa kuwa huriu unapaswa kuzingatia ukomo wa haki ya kupata habari kuwa
unakoma pale haki za watu wengine zinapoanzia.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii Peter
Serukamba amesema kuwa kamati yake imeufanyia kazi Muswada huo kupitia
maoni ya wadau na watu mbalimbali nchini ambayo ndio yamakuwa msingi wa
kuuboresha muswada huo.
Serukamba aliongeza kuwa kati ya
miswada ambayo wananchi wengi wameisoma na kusikilizwa ni Muswada habari
ambao umejadiliwa kwa njia mbalimbali ikiwemo vyombo vya habari; kwenye
magazeti, kwenye radio na Televisheni kupitia vipindi maalum vya
kujadili Muswada huu na maoni yao mengi yameingizwa kwenye Muswada huu”
alisema Serukamba.
0 maoni:
Chapisha Maoni