Na Mahmoud Ahmad Arusha
UMOJA wa vijana mkoa wa Arusha umelaani vikali kitendo cha
jenerali Twaha ulimwengu kumkashifu Rais Mstaafu na mwenyekiti wa CCM
taifa, Dkt Jakaya Kikwete kwa madai kuwa ashitakiwe mahakamani kwa
kutumia fedha za umma vibaya kwa kuanzisha mchakato wa katiba ambao
ulikwama kufikia tamati yake
Akitoa tamko hilio mbele ya wana habari mkoa wa Arusha
mwenyekiti wa umoja wa vijana mkoa wa Arusha Lengai Ole sabaya alisema
kuwa matamshi ya upotosha ji yaliyotolewa na jenerali twaha ulimwengu
ni ya kupotosha umma
Aliongeza kuwa kutokana na matamshi hayo UVCCM wanamtaka
jenerali aache kupotosha ukweli kama ulivyo kwani mchakato bado
haujakwama ila umezingwa na miingiliano ya vipindi vya uitishaji wa kura
ya maoni pamoja na kufanyika kwa uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.
Aidha idhini ya matumizi ya fedha za mchakato wa Katiba
ziliweza kuiidhinishwa na bunge kwa nia ya dhamira njema ya taifa ya
kuandika katika yake mpya na wala sio ubadilifu au matumizi mabaya kama
anavyotaka jenerali huyo.
Sabaya alisema kuwa alichokionesha jenerali mbele ya
kadamnasi na vyombo vya habari ni kejeli pamoja na dharau isiyo staili
kwani alionekana kujawa na nyongo kutokana na kumbukumbu zile za kuwekwa
kando na utawala wa mkapa kasha kuzikwa kwenye kaburi la sahau utawala
wa kikwete.
Aidha kutokana na matasmhi hayo umoja huo umewaomba na
kuwasihi watanzania kuwa makini na kutuipilia mbali sanjari na kuweka
tahadhari kwa watu wenye matamshi ya hamaki pamoja na hasira ambao wana
nia mbaya ya kubomoa taifa.
Kutokana na hilo pia umoja huo umesema kuwa
endapo kama ataendelea basi wao hawataweza kumtambua tena kama
mwanachama mwenzao na pia watashinikiza hata uanachama wake utiliwe
shaka kabisa
0 maoni:
Chapisha Maoni