Alhamisi, 9 Juni 2016

TUGHE Muhimbili Wapata Viongozi Wapya, Yaongeza Nafasi ya Vijana na Walemavu

H1Kaimu Mkurugenzi Mtendaji, Profesa Lawrence Museru wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) akizungumza na wajumbe wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali na Afya (TUGHE) wa tawi la hospitali hiyo kabla ya kufanyika kwa uchaguzi wa viongozi wa chama hicho leo kwenye ukumbi wa CPL, Muhimbili.
H2Wajumbe wa TUGHE katika hospitali hiyo wakipiga makofi leo baada ya Profesa Museru kuwaahidi kuwa ataboresha maslahi ya wafanyakazi hao ambao ni wajumbe wa chama hicho.
H3Mkurugenzi wa Rasilimali Watu, Makwaia Makani akiungana na wajumbe wa TUGHE wakati wakiimba nyimbo za mshikamano.
H4Wajumbe wa TUGHE wakiimba nyimbo za mshikamano leo kabla ya kuanza kwa uchaguzi wa viongozi wapya.
H5Katibu wa Tughe Mkoa wa Ilala Jijijini Dar es Salaam, Gaudence Kadiango akitoa maelekezo kabla ya kuanza kwa uchaguzi  wa viongozi wapya wa TUGHE leo.
H6Mmoja wa wajumbe wa TUGHE, Helmut Ngalawa akipiga kura leo kuchagua viongozi wapya wa chama hicho.
H7Baadhi ya wajumbe wakihesabu kura baada ya wajumbe kupiga kura leo kwenye ukumbi wa CPL-Muhimbili.
H8Aliyekuwa Mwenyekiti wa TUGHE katika Tawi la Muhimbili, Mziwanda Chimwege (kulia) na katibu wake, Faustine Kaitaba wakipongezana leo baada ya kuchaguliwa tena katika nafasi hizo kuongoza chama hicho kwa muda wa miaka mitano.
H9Mmoja wa wajumbe akimpongeza Mziwanda Chimwege kwa kuchaguliwa kuwa mwenyekiti wa TUGHE katika tawi la Muhimbili.10: Wajumbe wakishangilia baada ya viongozi waliowapigia kura kushinda uchaguzi huo leo.
H10 H11Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa hospitali hiyo, Profesa Museru, (wa pili kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wapya wa tawi la TUGHE Muhimbili akiwamo mwenyekiti, katibu na wajumbe wa halmashauri ya chama hicho.
Picha na JOHN STEPHEN, Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH).
…………………………………………………………………………………………………
Hospitali ya Taifa Muhimbili  (MNH) imepata viongozi wapya  wa Chama cha wafanyakazi wa Serikali  na Afya Tanzania (TUGHE),  Tawi la Muhimbili  katika uchaguzi uliofanyika leo majira ya alasiri katika ukumbi wa CPL hospitalini hapo .
Nafasi zilizogombaniwa  ni pamoja  na Mwenyekiti wa Tawi, Katibu wa Tawi, wajumbe wa Halmashauri ya Tawi, nafasi ya Mwenyekiti Kamati ya wanawake, Katibu kamati ya wanawake, Mjumbe kamati ya wanawake, Muweka Hazina kamati ya wanawake, nafasi ya  walemavu  pamoja na nafasi ya vijana.
Katika uchaguzi huo Bwana Mziwanda Salum Chimwege ametetea nafasi yake ya Uenyekiti wa tawi na kuibuka kidedea kwa kupata kura 248, huku nafasi ya Katibu ikichukuliwa na Bwana Faustine Fidelis Kaitaba ambaye amepata kura 215.
Walioshinda nafasi ya halmashauri ya tawi ni Idi  Shaweja,  Edina Maneno,  Seif  Athuman, Rama Sultan, Yusuph Mkando, Adam Alfan, Josephine Lwambuka, Shaban  Zubery, Isaya Mbinga, Charles Kayombo, Aly Mkali, Musa Mbuhita,Bure  Nasoro, Joyce Chirwa, Mecktidis Chonga, Aikael Kisanga, Hidal Mtoakani pamoja na Dk. Peter Kibacha.
Nafasi ya Mwenyekiti kamati ya wanawake imechukuliwa na Zainab  Mwagala  kwa kupata kura 71 huku Mwajuma Kisengo ameibuka mshindi kwa kupata nafasi ya Ukatibu kwa kupata kura 75 .
Muweka hazina kamati ya wanawake ni Halima Mayumana wakati nafasi ya vijana imechukuliwa na Husein Jalala Mkangazi ambapo  Salama Kasembe ameshinda nafasi ya walemavu.
Awali akifungua mkutano mkuu wa uchaguzi wa Tawi la TUGHE –Muhimbili  , Kaimu Mkurugenzi Mtendaji  wa  Hospitali ya Taifa Muhimbili-MNH- Profesa  Lawrence Museru ameupongeza uongozi uliopita wa TUGHE katika tawi hilo  kwa kushirikiana  vema na Menejimenti  pasipo migogoro.
Pamoja na mambo mengine Profesa Museru amewaeleza wajumbe wa mkutano huo kwamba kuanzia Julai mwaka huu MNH itaanza kutoa mkono wa heri kwa wastaafu wake sanjari na kutoa posho kwa watumishi wote wa hospitali hiyo.
“Posho hizi zinatolewa si kwamba hospitali ina pesa nyingi lakini  tunambua mchango wa ,  kwani  kila mmoja ametimiza  wajibu wake  hatua iliyochangia kuongeza mapato ya  hospitali  , hivyo nawasihi sana muendelee kufanya kazi kwa bidii ili suala hili liwe endelevu.”amesema Profesa Museru.
Pia ametumia fursa hiyo  kuwasisitiza  kwamba MNH itaendelea kuchua hatua kwa wafanyakazi wasiio waaminifu katika utoaji wa huduma .
Viongozi hao wa TUGHE tawi la Hospitali ya Taifa Muhimbili wataongoza kwa muda wa miaka mitan

0 maoni:

Chapisha Maoni