Tanzania ina upungufu wa maafisa ugani 6,266 ambao serikali inahitaji kuajiri kadri ya upatikanaji wa fedha.
Kauli hiyo imetolewa leo
Bungeni Dodoma na Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Mhe. Dkt. Charles
Tizeba wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum (CHADEMA), Mkoa wa
Kagera lililoulizwa kwa niaba yake na Mbunge wa Viti Maalum (CCM), Mkoa
wa Kagera, Mhe. Oliva Semuguruka aliyetaka kufahamu mpango wa serikali
katika kuwasaidia wakulima waweze kunufaika na kilimo cha Ndizi, Kahawa,
Mahindi na Maharage.
“Mathalani mwaka 2006 wizara
yangu ilibaini kuwa walikuwepo maafisa ugani 3,377, ukilinganishwa na
mahitaji ya maafisa hao 15,022″ alisema Dkt. Tizeba.
Aliongeza kuwa Serikali
inajitahidi kusomesha vijana wengi kwenye vyuo vya kilimo na kuajiri
maafisa ugani 5,377 na kufanya jumla ya wataalam kuwa 8,756 kwa sasa
ambao wanatoa elimu na kanuni bora za kilimo.
Tizeba alisema Serikali kwa
kushirikiana na Halmashauri za Wilaya, inaendelea kueneza matumizi ya
vituo vya rasilimali za Kilimo vya Kata ambapo jumla ya vituo 322
vimejengwa katika Halmashauri 106 kwenye mikoa 20.
“Kati ya vituo hivyo vituo 224
vimekamilika na vinafanya ya kutoa mafunzo kwa wakulima na wafugaji,
mashamba ya majaribio, kutoa huduma kwa wafugsjio na matumizi ya zana za
kilimo” alisema Dkt. Tizeba.
Aidha Waziri Tizeba aliongeza
kuwa Wizara yake inaandaa na kurusha vipindi vya redio kuhusu kanuni za
kilimo bora kupitia vituo mbalimbali vyas redio, ambapo kwa mwaka
2015/16 jumla ya vipindi 122 vilirushwa na vipindi 52 vilirushwa kupitia
TBC Taifa na vipindi 70 vilirushwa kupitia redio jamii.
Akijibu swali la nyongeza la
Mbunge wa Viti MaaluM (CCM), Mhe. Oliver Semguruka aliyetaka kujua ni
lini bei ya kahawa itapanda ili wakulima wasiuze nje ya nchi, Dkt Tizeba
alisema bei ya kahawa itakuwa nzuri ikiondolewa kodi 26 zilizopo hivi
sasa.
0 maoni:
Chapisha Maoni